Wakazi wakimbia mji wa Lebanon huku Israeli ikionya kufanya mashambulizi
Jeshi la Israel latoa agizo la kuhamishwa kwa mji wa kusini wa Tiro - ikiwa ni pamoja na sehemu ya Wakristo - likisema litachukua hatua "kwa nguvu".
Aliyekuwa Naibu Rais nchini Kenya Rigathi Gachagua, amesema kuwa atapinga uamuzi wa mahakama uliosema kuwa aliondolewa madarakani kwa njia ya halali na kusisitiza kuwa walitafsiri vibaya sheria na kulipa kishogo suala zima la haki.
Akisisitiza kuwa haki yake ya kusikilizwa ilikiukwa wakati wa mchakato huo, Gachagua ameahidi kuwasilisha pingamizi lake katika Mahakama ya Rufaa na vile vile, kutumia fursa zingine zote zilizopo ikiwa ni pamoja na Mahakama ya Juu Zaidi.
Gachagua alisema anaheshimu Idara ya Mahakama lakini hakubaliani na tafsiri ya mahakama kuhusu sheria katika kesi hiyo.
"Tutakata Rufaa katika Mahakama ya Rufaa juu ya uamuzi huo na tunatumai haki itapatikana," alisema.
Gachagua alisema haki haikuzingatiwa wakati wa mchakato wa kuondolewa madarakani.
"Kanuni ya muda mrefu ya kisheria ya utaratibu wa haki na haki ya kusikilizwa bila upendeleo imetupiliwa mbali na kupuuzwa mchana kweupe. Ni siku ya huzuni iliyoje kwa wale ambao wamepitia haya siku za nyuma na wale ambao wanakabiliwa na hali kama hiyo siku zijazo," alisema.
Haya yanajiri baada ya majaji watatu wa Mahakama Kuu kutoa uamuzi jana Jumatatu kwamba mchakato wa kumuondoa madarakani kwenye Bunge na Seneti ulikuwa halali na kwamba matokeo hayo yalisalia kuwa halali kwa mujibu wa Katiba.
Je, huu ndio mwisho wa Rigathi Gachagua katika siasa za Kenya?
Gachagua apata pigo huku Mahakama Kuu ikitupilia mbali ombi la kupinga kuondolewa madarakani
📌 Kaynak
Bu özet BBC Swahili kaynağından otomatik derlenmiştir. Tamamı için orijinal habere gidin.
Orijinal haberi oku →