Kwa nini Iran iliamua kuishambulia Israel?

📌 Diğer 📰 BBC Swahili 🕐 3 saat önce
Kwa nini Iran iliamua kuishambulia Israel?

Kwa mujibu wa taarifa za maafisa wa kijeshi nchini Iran, shambulio hilo lilikuwa la " kulipiza kisasi mashambulizi ya Israel dhidi ya vitongoji vya Beirut."

Baada ya miezi kadhaa ya usitishaji mapigano uliokumbwa na visa vya Iran na Marekani kushambuliana hapa na pale, makombora ya balistiki ya Iran yalirushwa tena Jumapili jioni kuelekea maeneo kadhaa nchini Israel.

Tukio ambalo, kwa mujibu wa taarifa za maafisa wa kijeshi nchini Iran, lilikuwa hatua ya " kulipiza kisasi mashambulizi ya Israel dhidi ya vitongoji vya Beirut."

Ingawa maafisa wa Iran walidai tangu mwanzo wa usitishaji vita kwamba mpango huo mpya wa maelewano utajumuisha pia Lebanon, Israel haikuwahi kuzingatia kipengele hiki, na katika kipindi hiki, ilishambulia maeneo kadhaa nchini humo.

Wiki iliyopita, Israel ilitangaza kuwa itafanya mashambulizi makubwa katika vitongoji vya kusini mwa Beirut. Lakini Tehran ilitishia kuchukua hatua operesheni hiyo ikitekelezwa. Na hapo ndipo Rais wa Marekani Donald Trump alipoitaka Israel kutoishambulia Lebanon hadharani.

Trump aliandika katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii wa Truth Social kwamba amewahakikishia Israel na maafisa wa Hezbollah kupitia mawasiliano ya simu kwamba hakuna shambulio lolote litakalofanywa na pande zote mbili.

Tukio ambalo baadhi ya vyombo vya habari na wachambuzi walio karibu na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wamelitafsiri kuwa ni ishara ya mafanikio ya tishio la Tehran.

Lakini hali ya utulivu ulidumu kwa siku chache kabla ya Jeshi la Israel kutangaza Jumapili mchana kwamba limeshambulia maeneo kadhaa viungani mwa Beirut. Ingawa haijabainika ni watu wangapi waliouawa au kujeruhiwa katika shambulio hilo, mamlaka nchini Iran ilijibu hatua hiyo kurusha msururu wa makombora kuelekea Israel.

Awali Mohammad Baqer Qalibaf aliandika kwenye akaunti yake ya X-Net: "Hawazingatii makubaliano ya usitishaji vita wala hawatilii maanani mazungumzo ya amani. Kwa kuendelea kutekeleza kizuizi cha majini na ukiukaji wa makubaliano kuhusu Lebanon, walionyesha kwamba wanaelewa tu lugha ya kutumia nguvu."

Tangu wakati huo, baadhi ya waangalizi wametabiri kuwa Iran huenda ikaamua kujibu hatua hiyo ya Israel.

Chanzo cha picha, Hamed Malekpour - ICANA News Agency via Getty Images

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Tangu kuuawa kwa Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, baadhi ya viongozi wakuu katika serikali ya Iran wameonekana kutafakari upya mafundisho ya kijeshi na usalama wa nchi hiyo.

Baadhi ya wachambuzi wanaamini kwamba misimamo ya Tehran baada ya vita vya siku 12 ikifuatiwa na vile vya siku 40 vimefichua dalili ya mabadiliko haya. Katika miaka ya mwisho ya serikali ya Ali Khamenei, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilijaribu kujiepusha na mgo

📌 Kaynak

Bu özet BBC Swahili kaynağından otomatik derlenmiştir. Tamamı için orijinal habere gidin.

Orijinal haberi oku →
📱
News AI World — Mobil uygulama
Bu haberleri 45 dilde, anlık çeviriyle cebinde. Erken erişim için Gmail adresini bırak.
← Tüm haberlere dön