Gachagua apata pigo huku Mahakama Kuu ikitupilia mbali ombi la kupinga kuondolewa madarakani

📌 Diğer 📰 BBC Swahili 🕐 21 saat önce
Gachagua apata pigo huku Mahakama Kuu ikitupilia mbali ombi la kupinga kuondolewa madarakani

Akitoa uamuzi huo kwa niaba ya jopo la majaji watatu, Jaji Eric Ogola alishikilia kuwa ushiriki wa kisiasa na maoni ya wabunge peke yake, hakuwezi kuthibitisha kuwa ni upendeleo wa kikatiba.

Aliyekuwa Naibu Rais nchini Kenya Rigathi Gachagua amepata pigo baada ya Mahakama Kuu kutupilia mbali kesi aliyowasilisha na kutoa uamuzi kuwa Bunge lilichukua hatua kulingana na Katiba ya nchi kumuondoa madarakani.

Uamuzi huo uliotolewa na majaji watatu, ulitupilia mbali ombi la Gachagua la kupinga kuondolewa kwake madarakani, na kusema kuwa Bunge la Taifa pamoja na Seneti walifuata sheria na kwamba walimpa fursa ya kujitetea kutokana na hoja zilizowasilishwa dhidi yake.

Majaji hao pia walisema kwamba ushirikishi wa umma uliofanywa kabla ya Gachagua kuondolewa madarakani kulizingatia Katiba na kwamba Bunge lilikuwa na haki ya kutekeleza jukumu lake la kusimamia, kufuatilia na kutathmini maafisa wa serikali.

Uamuzi huo umetolewa katika moja ya kesi za kihistoria ya kisiasa nchini Kenya na kuthibitisha kuwa Gachagua aliondolewa afisini kihalali.

Katika uamuzi wa awali, mahakama ilisema kwamba hakukuwa na ushahidi ulioonyesha kuwa kulikuwa na upendeleo, maamuzi yaliyopangwa mapema au mgongano wa kimaslahi katika mchakato wa kumtimua madarakani Rigathi Gachagua.

Akitoa uamuzi huo kwa niaba ya jopo la majaji watatu, Jaji Eric Ogola ameshikilia kuwa ushiriki wa kisiasa na maoni ya wabunge peke yake, hakuwezi kuthibitisha kuwa ni upendeleo wa kikatiba.

"Ukweli kwamba Wabunge waliunga mkono au kupinga kuondolewa madarakano kwa Mheshimiwa Gachagua hakuwezi, kujisimamia, kuthibitisha kuwa ni upendeleo wa kikatiba," mahakama ilisema.

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Jaji alisisitiza kuwa kuondolewa madarakani ni mchakato wa kawaida wa kisiasa na kikatiba ambapo wabunge hawatarajiwi kuangazia hoja iliyowasilishwa mbele yao bila kufahamu suala husika au maoni ya kisiasa.

Kinachotakiwa kwa mujibu wa Katiba, mahakama ilisema, si kukosekana kwa mielekeo ya kisiasa bali kuwepo kwa ushirikiano wa nia njema na ushahidi na hoja wakati wa mchakato.

"Kile ambacho Katiba inahitaji ni uwepo wa uwazi wakati wa kusikiliza ushahidi, kusikiliza hoja, na kutekeleza wajibu wao wa kikatiba kwa uaminifu na ndani ya mipaka ya kikatiba", hakimu amesema.

Kwa msingi huo, mahakama ilikataa madai ya mlalamikaji kwamba wabunge walikuwa wamefanya maamuzi mapema au walishawishiwa na mgongano wa maslahi, na kusema kuwa madai hayo hayakuwa na ushahidi wa kutosha.

"Hivyo basi, madai ya upendeleo, kwamba kulikuwa na uamuzi uliofanywa mapema, na mgongano wa kimaslahi yaliyowasilishwa na mlalamishi dhidi ya Maspika, Wabunge na Maseneta, kulingana na nyaraka mbele ya Mahakama hii, ni madai yasiyo na uthibitisho yaliyoegemea tuhuma za kisiasa na

📌 Kaynak

Bu özet BBC Swahili kaynağından otomatik derlenmiştir. Tamamı için orijinal habere gidin.

Orijinal haberi oku →
📱
News AI World — Mobil uygulama
Bu haberleri 45 dilde, anlık çeviriyle cebinde. Erken erişim için Gmail adresini bırak.
← Tüm haberlere dön