Trump: Iran imechelewa kufikia makubaliano na Marekani, sasa italipa gharama

📌 Diğer 📰 BBC Swahili 🕐 6 saat önce
Trump: Iran imechelewa kufikia makubaliano na Marekani, sasa italipa gharama

Kauli ya Rais wa Marekani DonalD Trump inajiri baada ya Iran kusema itatathmini upya hatima ya mazungumzo baada ya mashambulizi mapya ya Marekani.

"Kila kitu tayari kimejadiliwa kikamilifu na kukamilishwa. Tuna makubaliano yaliyokamilika baada ya mazungumzo ya kina, lakini Iran wanaendelea kuchelewesha," asema Trump.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Iran, ujumbe wa ngazi ya juu kutoka Qatar umewasili Tehran mchana wa leo kwa mazungumzo na maafisa wa Iran.

Gazeti la serikali ya Iran limeripoti kuwa ujumbe huo umefika kwa lengo la kujadili uhusiano wa pande mbili pamoja na hali ya usalama na maendeleo ya kisiasa katika eneo la Mashariki ya Kati.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wajumbe hao pia wanatarajiwa kujadiliana kuhusu hatua za kidiplomasia zinazolenga kumaliza mzozo unaoendelea kati ya Marekani na Iran, sambamba na masuala ya ushirikiano wa nchi hizo mbili na maendeleo ya kikanda.

Ziara hiyo inafanyika wakati mvutano kati ya Marekani na Iran ukiendelea kuongezeka kufuatia kuangushwa kwa helikopta ya kijeshi ya Marekani, tukio ambalo limechochea mashambulizi na hatua za kulipizana kati ya pande hizo mbili.

Mapema leo, Donald Trump alisema Iran imechelewesha kwa muda mrefu mazungumzo na sasa italazimika "kulipa gharama" ya hatua hiyo.

Kwa upande wake, Iran imesema itafanya tathmini upya kuhusu kuendelea na mazungumzo hayo kufuatia mashambulizi mapya ya Marekani.

Iwapo Iran na Marekani wataafikia makubaliano, Israel itakuwa na chaguo gani?

Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema Iran imechelewa mno kufikia makubaliano na Marekani na sasa italazimika “kulipa gharama” ya kuchelewa huko.

Katika ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wake wa Truth Social Jumatano, Trump amesema Iran imepata pigo kubwa na kwamba imebaki kutoa matamshi pekee bila kuchukua hatua za maana.

"Mnyanyasaji wa Mashariki ya Kati sasa ameshindwa," alisema Trump.

Aliongeza kuwa Iran ilichelewesha kwa muda mrefu kufikia makubaliano ambayo, kwa mujibu wake, yangekuwa na manufaa makubwa kwa taifa hilo.

"Walichelewa mno kufikia makubaliano ambayo yangekuwa bora kwao. Sasa watalazimika kulipa gharama yake," alisema.

Kauli hiyo imekuja huku mvutano kati ya Iran na Marekani ukiendelea kuongezeka tangu Jumatano asubuhi, ambapo pande zote mbili zimedai kufanya mashambulizi dhidi ya malengo ya upande mwingine.

Mapema leo, Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani Mashariki ya Kati (CENTCOM) ilisema vikosi vyake vilichukua hatua za kijeshi dhidi ya Iran kujibu kuangushwa kwa helikopta ya kijeshi ya Marekani.

"Operesheni hii ni jibu kwa uchokozi wa Iran ambao haukuchochewa," ilisema CENTCOM katika taarifa yake.

Kwa upande wake, Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu wa Iran walidai kuwa Marekani ilifanya mashambulizi dhidi ya maeneo kadhaa ya J

📌 Kaynak

Bu özet BBC Swahili kaynağından otomatik derlenmiştir. Tamamı için orijinal habere gidin.

Orijinal haberi oku →
📱
News AI World — Mobil uygulama
Bu haberleri 45 dilde, anlık çeviriyle cebinde. Erken erişim için Gmail adresini bırak.
← Tüm haberlere dön