Ronaldo na Messi - Ushindani ambao ulitawala soka kwa miongo miwili - lakini nani bora zaidi kati yao?

📌 Diğer 📰 BBC Swahili 🕐 7 saat önce
Ronaldo na Messi - Ushindani ambao ulitawala soka kwa miongo miwili - lakini nani bora zaidi kati yao?

Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wamekuwa kileleni mwa mchezo wa kandanda kwa miaka 20 iliyopita. BBC Michezo inaangazia ushindani huu ambao umeibua soka.

Kaka wa Brazil ndio mwanzo alikuwa ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Fifa 2007 lakini hafla ya kuwazawadia washindi zawadi zao ilizua gumzo lililoishia kuwa ushindani katika historia ya soka.

Lionel Messi na Cristiano Ronaldo walikuwa wamemaliza wa pili na wa tatu mtawalia lakini nguli wa Brazil Pele alimpa mshindi wa pili zawadi ya nafasi ya tatu kwenye Jumba la Opera mjini Zurich.

Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) Sepp Blatter alilazimika kuingilia kati tukio hilo na kuwaambia wawili hao kubadilishana tuzo hizo, na walionekana kutoridhithishwa na hatua hilo.

Kwa miaka 10 iliyofuata, Messi au Ronaldo walishinda kila tuzo ya Ballon d'Or na Fifa. Tangu 2007, matuzo 20 kati ya 29 zilizotunukiwa mchezaji bora wa mwaka wa Ulaya iliemuendea mmoja wao.

Huku kila mmoja wao akikaribia kufunga mabao 2,000, kushinda mataji 85 ya klabu na nchi na tuzo nyingi za watu binafsi, Messi na Ronaldo daima watakumbukwa kama wachezaji wawili waliotunikiwa zaidi katika historia.

Ni mchuano ambao umefafanua miongo miwili iliyopita ya kandanda, vilabu, nchi na mashindano yaliyopita ili kurekebisha jinsi mchezo ulivyochezwa, kutumiwa na kujadiliwa kote ulimwenguni.

"Wachezaji wawili kama wao, wanaoshindana katika kiwango hicho kwa miaka mingi, wakipigania Ballon d'Or na kufunga mabao mengi kiasi hicho... sidhani kama tutaiona tena," mshindi wa Kombe la Dunia la Argentina Angel di Maria, ambaye alicheza na wote wawili, anasema katika kipindi kipya cha BBC Sport Rivals: Messi v Ronaldo.

Wakisukumwa naari ya kushinda mataji, na hamu ya kudumu ya kuwa mchezaji bora zaidi, wawili hao - ambao huenda wanacheza mechi zao za mwisho za Kombe la Dunia msimu huu wa joto - ushindani wao umefikia kiwango kipya.

Ni ushindani ambao ni zaidi ya mjadala wa mchezaji 'bora wa wakati wote' ambao walichochea.

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Ukimuuliza mtu yeyote ni mchezaji gani bora zaidi kati ya Messi na Ronaldo huenda usipate jibu kutokana na mjadala utakaoibuka.

"Bila shaka ni Ronaldo," mchezaji mwenzake wa zamani wa Manchester United Rio Ferdinand anasema.

"Messi ndiye bora zaidi hana mshindani," anasisitiza mchezaji na meneja wa zamani wa Barcelona Xavi.

Ronaldo amekuwa na maoni yake siku za nyuma, akisema mwaka 2012: "Huwezi kulinganisha Ferrari na Porsche. Ni injini tofauti. Baadhi ya watu wanasema mimi ni bora zaidi, wengine wanasema yeye. Wataamua nani bora kwa sasa na nadhani ni mimi."

Takwimu zinasema nini? Ikiwa itaamuliwa kwa mabao au mataji ya Ligi ya Mabingwa, Ronaldo anaongoza. Ikiwa ni Ballons d'Or au jumla

📌 Kaynak

Bu özet BBC Swahili kaynağından otomatik derlenmiştir. Tamamı için orijinal habere gidin.

Orijinal haberi oku →
📱
News AI World — Mobil uygulama
Bu haberleri 45 dilde, anlık çeviriyle cebinde. Erken erişim için Gmail adresini bırak.
← Tüm haberlere dön