Marekani na Iran zashambuliana Mashariki ya Kati kwa siku ya pili mfululizo
Iran inasema ilijibu mashambulizi ya Marekani kwa kulenga mali za Marekani katika nchi za Kuwait, Jordan na Bahrain, iliyoripoti uharibifu katika mji mkuu usiku kucha.
Mjadala unaendelea kati ya Iran na Marekani kuhusu kufungwa kwa Mlango-Bahari wa Hormuz.
Siku ya Jumatano, vyombo vya habari vya serikali ya Iran viliripoti kwamba njia yenye shughuli nyingi ya usafirishaji wa meli "imefungwa kabisa kwa kila aina ya meli".
Siku ya Alhamisi asubuhi, mamlaka ya njia za maji ya Iran imesema tena mlangobahari huo umefungwa, vyombo vya habari vya serikali vinaripoti, kufuatia wimbi jipya la mashambulizi ya Marekani hapo jana.
Hata hivyo, usiku kucha, Kamandi Kuu ya Marekani ilikanusha kuwa njia hiyo imefungwa, na kusema: "Meli za kibiashara zinaendelea kusafiri ndani na nje ya Mlango-Bahari wa Hormuz usiku wa leo."
Mlango-Bahari wa Hormuz unasalia kuwa kitovu cha mazungumzo, huku Marekani na Iran zikijaribu kudhibiti mustakabali wake.
Iran imekuwa ikifunga njia hiyo tangu vita vilipoanza na kuwaacha maelfu ya mabaharia wakiwa wamekwama, huku Marekani ikiweka vizuizi kwenye bandari za Iran kama njia ya kulipiza kisasi.
Iran imetengeneza Mamlaka ya Mlango-Bahari wa Ghuba ya Uajemi, ambayo inasema itaruhusu jeshi la Iran kusimamia meli zinazopita baada ya vita.
Lakini Marekani inasisitiza kwamba Iran haitaruhusiwa kudhibiti mlangobahari baada ya vita - Donald Trump alidai Jumatano kwamba jeshi la Marekani lilisaidia meli 200 za kibiashara kupita kwenye njia hiyo ya majini kama sehemu ya "misheni ya siri".
Mythos ni nini na kwa nini inaonekana kuwa tishio kubwa kuliko Mlango bahari wa Hormuz?
Jinsi Iran Ilivyogeuza Mlango wa Hormuz kuwa silaha yenye nguvu zaidi duniani
📌 Kaynak
Bu özet BBC Swahili kaynağından otomatik derlenmiştir. Tamamı için orijinal habere gidin.
Orijinal haberi oku →