'Ndoa ya pamoja' ilivyotibuka: Mabwana harusi 42 walifika, mabibi harusi hawakujitokeza

📌 Diğer 📰 BBC Swahili 🕐 2 saat önce
'Ndoa ya pamoja' ilivyotibuka: Mabwana harusi 42 walifika, mabibi harusi hawakujitokeza

Waliambiwa kwamba wangefunga ndoa ndani ya saa 24 zijazo. Lakini maharusi hawakujitokeza na hivyo ndivyo halfla hiyo ilivyotibuka.

Makumi ya wanaume wametapeliwa katika mojawapo ya kashfa ya ulaghai wa ndoa nchini India. Wanaume hao waliokuwa wamesafiri hadi mji wa Dewas katika jimbo la Madhya Pradesh wakiwa na matumaini ya kufunga ndoa waligundua, baada ya kusubiri kwa saa kadhaa, kwamba walikuwa waathirika wa mtandao uliopangwa waulaghai.

Asubuhi ya Mei 24, hekalu la Mata Tekri mjini Dewas ilikuwa imepambwa tayari kwa sherehe kubwa ya harusi. Wanaume kutoka miji na vijiji mbalimbali, baadhi yao wakiwa na jamaa zao, wengine wakiwa na magari ya kukodi, walikuwa wamefika kwenye ukumbi huo. Wengi wao walikuwa wamevalia mavazi ya harusi, tayari kwa moja ya siku muhimu zaidi maishani mwao.

Waliambiwa kwamba wangefunga ndoa ndani ya saa 24 zijazo. Lakini maharusi hawakujitokeza na hivyo ndivyo halfla hiyo ilivyotibuka.

Kwa mujibu wa polisi, kilichotokea huko Dewas ni ulaghai ulioenea uliojificha kama "ndoa ya pamoja"; mpango ambapo wanaume wanaotafuta wake walitozwa kiasi kikubwa cha pesa kwa ahadi za uwongo.

Naibu Kamishna wa Polisi wa Dewas, Jivirsen Bhadriya, alisema uchunguzi umebaini kuwa watu wengi wamekuwa wakilengwa katika kashfa hiyo. Watu wawili wamekamatwa kufikia sasa na uchunguzi unaendelea ili kuwabaini na kuwakamata washtakiwa wengine katika kesi hiyo.

Kulingana na polisi na waathiriwa, kashfa hiyo ilipangwa kwa uangalifu. Wanachama wa mtandao huo kwanza waliwatambua wanaume wanaotafuta wake na kisha kuwafahamisha kwamba wasichana wanaoishi katika kituo cha kidini katika jiji la Indore walikuwa tayari kwa ndoa.

Katika hatua iliyofuata, fedha zilikusanywa kutoka kwa waliowasilisha maombi kwa kisingizio cha usajili, kuandaa hati, na kukamilisha taratibu za kisheria. Hatua zote zilifanywa kupitia simu za rununu na mtandao.

Ili kupata imani zaidi, picha za wasichana hao zilitumwa kwa familia; picha hizo baadaye zilibainika kuwa zilikusanywa kutoka kwenye mitandao ya kijamii na hazikuwa na uhusiano wowote na tukio hilo.

waathiriwa wa ome pia wanasema kwamba jina la waziri mkuu wa serikali lilitumika kunadi mpango huo. Waliambiwa kwamba maafisa wa serikali wangehudhuria sherehe hiyo na kwamba msaada maalum wa kifedha ungetolewa kwa wanandoa hao.

Mmoja wa vijana ambaye alikuwa mwathirika wa tukio hilo anasema: "Tuliambiwa kwamba wasichana walikuwa katika hali nzuri sana na tayari kuolewa. Kila kitu kilionekana kuwa sawa kiasi kwamba hatukuwa na sababu ya kuwatilia shaka."

Anaeleza kuwa alipoomba kukutana na msichana aliyemchagua, aliambiwa kuwa kwa kuwa wasichana hao walikuwa wakikaa kwenye makazi ya kidini, mkutano wa kabla ya harusi haukuwezekana. Badala yake, alihaki

📌 Kaynak

Bu özet BBC Swahili kaynağından otomatik derlenmiştir. Tamamı için orijinal habere gidin.

Orijinal haberi oku →
📱
News AI World — Mobil uygulama
Bu haberleri 45 dilde, anlık çeviriyle cebinde. Erken erişim için Gmail adresini bırak.
← Tüm haberlere dön