Bowen: Trump na Netanyahu walitaka kubadilisha mwelekeo wa Mashariki ya Kati - sasa wanakabiliwa na tishio

📌 Diğer 📰 BBC Swahili 🕐 2 saat önce
Bowen: Trump na Netanyahu walitaka kubadilisha mwelekeo wa Mashariki ya Kati - sasa wanakabiliwa na tishio

Viongozi wa Marekani na Israel wamepoteza udhibiti wa mzozo wa Iran baada ya kukosea ahesabu ya tathmini yao.

Donald Trump na Benjamin Netanyahu wanaamini ushindi dhidi ya Iran kutabadilisha muelekeo wa Mashariki ya Kati.

Eneo hilo linabadilika. Lakini sio kwa jinsi walivyotarajia. Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran haijasalimu amri. Hatari inayowakodolea macho sasa kuibuka kwa mzozo wa mara kwa mara.

Utawala wa Iran umedhihirisha wazi kwamba sio rahisi kuusambaraisha kama walivyodhani Trump and Netanyahu. Mtazamo wao haukuwa sahihi na sasa wameshindwa kudhibiti matokeo ya hatua yao dhidi ya taifa hilo.

Tukio la hivi punde ni la Iran kuangusha helikopta ya Marekani aina ya Apache. Hii inaashiria kuwa watawala wa Iran bado wanaweza kuwadhuru Wamarekani bila kulegeza msimamo wao katika juhudi za kuibuka washindi katika mgogoro unaoendelea.

Rais na majenerali wake watajaribu kujibu hatua ya Iran, ili kuonyesha kwamba hatakubali kuhangaishwa, huku wakijizatiti wakidumisha mchakato wa kidiplomasia usio na tija. Wahudumu wa Apache walinusurika. Laiti wangeuawa, jibu la Marekani huenda lingelikuwa kali zaidi.

Trump amekuwa akitegemea makubaliano na Iran ya kufungua tena Mlango-Bahari wa Hormuz na kukubaliana na masharti ya mazungumzo ya muda mrefu kuhusiana na masuala makubwa, ikiwa ni pamoja na hifadhi ya urani iliyorutubishwa ya Iran na mipango yake ya nyuklia.

Wamarekani wanapinga vikali vita hivyo, sasa Trump anataka kujiondoa kwa kutafuta njia ambayo anaweza kuiwasilisha kama ushindi. Hii inaonekana kuwa changamoto kubwa.

Trump na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wamepata funzo la zamani.

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Tangu wanadamu walipogundua vita, viongozi wamebaini kwamba ni rahisi kuanzisha vita kuliko kumaliza vita kwa ushindi wa moja kwa moja.

Walipoyaelekeza mataifa yao kwenye vita dhidi ya Iran siku ya mwisho ya mwezi Februari, wawili hao walitoa taarifa za video kwa kutumia maneno yaliyoakisi dhana kwamba wakati wa mabadiliko ya kihistoria unawadia. Utawala ambao umekuwa umadarakani nchini Iran tangu kupinduliwa kwa Shah mnamo 1979 ulikuwa unaelekea kuondolewa mamlakani.

"Kwa watu watukufu wa Iran, Ninasema usiku wa leo kwamba wakati uhuru wanu inanukia. Endelea kujikinga. Msiondoke majumbani mwenu. Nje ni hatari sana. Babomu yatadondoshwa kila mahali. Tutakapomaliza, chukueni serikali yenu. Hii huenda ikawa furasa ya kipekee kwa vizazi vijavyo."

Asubuhi iliyofuata, Netanyahu alisimama kwenye mwanga wa jua juu ya paa la Kyria, jumba la wizara ya ulinzi ya Israel lililopo katikati mwa jiji la Tel Aviv, ili kurekodi hotuba yake. Sawa na alivyofanya Trump, alizungumza kana kwamba ana hakika ya ku

📌 Kaynak

Bu özet BBC Swahili kaynağından otomatik derlenmiştir. Tamamı için orijinal habere gidin.

Orijinal haberi oku →
📱
News AI World — Mobil uygulama
Bu haberleri 45 dilde, anlık çeviriyle cebinde. Erken erişim için Gmail adresini bırak.
← Tüm haberlere dön