Meli ya tatu ya mafuta yashambuliwa karibu na Oman
Marekani inasema meli iliyokuwa na bendera ya Guinea-Bissau, Jalveer, "ilikiuka masharti yaliyowekwa".
Marekani imethibitisha kuwa ilifanya shambulizi kwenye meli ya M/T Jalveer yenye bendera ya Guinea-Bissau.
Kamandi Kuu ya Marekani (Centcom) inasema meli hiyo "ilikiuka kizuizi" kwa kujaribu kusafirisha mafuta ya Iran kupitia Ghuba ya Oman.
India yaishutumu Marekani kwa kuishambulia meli ya tatu iliyokuwa na mabaharia wake
Wakati huo huo, Wizara ya mambo ya nje ya India imeishutumu Marekani kwa kuishambulia meli ya tatu iliyokuwa imewabeba mabaharia wa India karibu na bandari ya Shinas ya Oman asubuhi ya leo.
Meli ya M/T Jalveer, yenye bendera ya Guinea-Bissau, ilikuwa na mabaharia 20 wa India ndani yake, ambao wote wanaripotiwa kuwa salama, kulingana na wizara ya meli ya India, ambayo inasema uokoaji bado unaendelea.
Katika mkutano na waandishi wa habari mjini New Dehli asubuhi ya leo, wizara ya mambo ya nje ilisema mashambulizi matatu tofauti kwenye meli za Settebello, Marivex na Jalveer " yamefanywa na Jeshi la Wanamaji la Marekani".
Kamandi Kuu ya Marekani (Centcom) imethibitisha mashambulizi dhidi ya meli Settebello na Marivex.
Mawaziri waliongeza kuwa meli 13 zenye bendera ya India na zaidi ya mabaharia 18,000 wa India walikuwa wamekwama katika eneo la Ghuba, wakiwemo 562 kwenye meli zenye bendera ya India.
Bowen: Trump na Netanyahu walitaka kubadilisha mwelekeo wa Mashariki ya Kati - sasa wanakabiliwa na tishio
Marekani yashambulia meli ya Iran katika Ghuba ya Oman - ripoti
Mabaharia watatu wa India wauawa katika shambulio la Marekani karibu na Oman
📌 Kaynak
Bu özet BBC Swahili kaynağından otomatik derlenmiştir. Tamamı için orijinal habere gidin.
Orijinal haberi oku →