Kombe la Dunia 2026: Mexico v Afrika Kusini tufuatilie moja kwa moja

📌 Diğer 📰 BBC Swahili 🕐 2 saat önce
Kombe la Dunia 2026: Mexico v Afrika Kusini tufuatilie moja kwa moja

Pazia la mashindano ya Kombe la Dunia 2026 linafunguliwa leo. Mechi ya ufunguzi ni kati ya Mexico na wawakilishi wa Afrika, timu ya taifa ya Afrika Kusini saa nne kamili usiku

Mwanamuziki maarufu wa Colombia Shakira ataimba wimbo wake rasmi kwa ajili ya Kombe la Dunia la 2026 katika sherehe za ufunguzi za mashindano hayo nchini Mexico.

Shakira atatumbuiza wimbo wa Dai Dai, pamoja na Burna Boy, katika uwanja wa Estadio Azteca mjini Mexico City, kabla ya mchezo kati ya Mexico na Afrika Kusini, moja kati ya michezo 104 ya mashindano hayo.

Dai Dai - ni msemo wa Kiitaliano unaomaanisha "twende" au "njoo".

Mwanamuziki wa reggaeton wa Colombia J Balvin na msanii nyota wa Afrika Kusini Tyla pia watatumbuiza kwenye ufunguzi huo nchini Mexico.

Sherehe za ufunguzi zitafanyika kabla ya kila mchezo wa kwanza unaochezwa katika mataifa wenyeji ya Marekani, Kanada na Mexico.

Nchini Canada, wasanii Michael Buble na Alanis Morissette wataongoza sherehe za ufunguzi katika Uwanja wa BMO huko Toronto kabla ya Canada kucheza na Bosnia na Herzegovina siku ya Ijumaa, 12 Juni.

Nchini Marekani, mwanamuziki maarufu Katy Perry na rapa Future watatumbuiza kabla ya Marekani kucheza na Paraguay katika Uwanja wa SoFi huko Los Angeles siku ya Ijumaa, 12 Juni kwa huko Marekani, saa 10 alfajiri ya Jumamosi kwa saa za Afrika Mashariki).

📌 Kaynak

Bu özet BBC Swahili kaynağından otomatik derlenmiştir. Tamamı için orijinal habere gidin.

Orijinal haberi oku →
📱
News AI World — Mobil uygulama
Bu haberleri 45 dilde, anlık çeviriyle cebinde. Erken erişim için Gmail adresini bırak.
← Tüm haberlere dön