Kombe la Dunia 2026: Ufaransa inaongeza 3- 1 Senegal
Usiku huu Senegal wanakutana na Ufaransa
Kylian Mbappe sasa ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Les Bleus, akimpita Olivier Giroud.
Dakika chache baada ya Senegal kufunga goli la kufutia machozi , nahodha wa Ufaransa Kylian Mbappe apiga shuti kali hadi wavuni
Deschamps anastahili pongezi kubwa kwa mabadiliko aliyoyafanya kipindi cha mapumziko. Alibadilishwa kutoka 4-4-2 hadi 4-4-1-1 . Alimsogeza Dembele kulia hatua ambayo ilimruhusu kutoa kusababisha mashambulizi zaidi . Alimsogeza winga wake wa kushoto karibu na goli.
Ufaransa inadhibiti mchezo kikamilifu sasa. Senegal hawana majibu yoyote.
Pat Nevin Winga wa zamani wa Scotland kwenye BBC Radio 5 Live katika Uwanja wa New York New Jersey
Alan Shearer Mshambulizi wa zamani wa Uingereza kwenye BBC One
Ufaransa inaonekana timu tofauti kabisa baada ya kipindi cha kwanza .
Mabadiliko maradufu kwa Senegal. Ismaila Sarr na Lamine Camara wanatoa nafasi kwa Ibrahim Mbaye wa PSG na Habib Diarra wa Sunderland.
kwa bao hilo Kylian Mbappe anakuwa mfungaji bora zaidi wa Ufaransa pamoja na Olivier Giroud.
Pia amebakisha mabao matatu pekee kumfikia Miroslav Klose wa Ujerumani aliyeweka rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi kwenye Kombe la Dunia
Kylian Mbappe anakimbia kwa ustadi kufikia mpira uliopigwa na Michael Olise na kumtungua Edouard Mendy bila shida.
Kipindi cha pili kinaendelea sasa . Timu zimeanza kufunguka, huenda tukashuhudia goli wakati wowote
Ian Dennis BBC Radio 5 Live mwandishi mwandamizi wa kandanda katika New York New Jersey Stadium
Dayot Upamecano na Jules Kounde wanaonekana kuwa na mabishano kidogo. Wamekuwa wazembe.
Hadi kufikia sasa hawajafanya mashambulizi yoyote katika lango la Senegal
Alan Shearer: Mshambulizi wa zamani wa Uingereza kwenye BBC One anasema:
"Mtu anayepaswa kufanya vizuri zaidi ni Mbappe. Amepata mipira mara nne na kupoteza mara tatu. Hilo ndilo lililopeleka nafasi hiyo kwa Jackson ambaye alikaribia kuifungia Seenegal, alipoteza mpira kirahisi, Senegal ikauchukua na kupeleka mashambulizi mbele na Ufaransa wakakoswakoswa"
Kikosi cha Ufaransa kina kasi ya hali ya juu kiasi kwamba wakati mwingine ni vigumu kuelewa
Tchouameni anashuka kwenye safu ya ulinzi wakati Ufaransa ina mpira na kuunda safu ya nyuma ya wachezaji watatu na mabeki wawili wa kati.
Winga wa kulia Olise na mshambuliaji Ousmane Dembele wanapokezana kushuka chini kila mara, waktengeneza nafasi ya kuonekana kupokea mipira kwenye sehemu ya kiungo wa chini .
📌 Kaynak
Bu haber XML kaynağından derlenmiştir. Tamamı için orijinal habere gidin.
Orijinal haberi oku →