Waridi wa BBC: "Mazishi yangu tayari yalikuwa yameandaliwa" asimulia mwanamke anayeishi na Virusi vya HIV

📰 Gündem 📰 Kenya 🕐 5 saat önce
Waridi wa BBC: "Mazishi yangu tayari yalikuwa yameandaliwa" asimulia mwanamke anayeishi na Virusi vya HIV

Kipindi hicho Margret anapatikana na virusi vya HIV, dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa ukimwi yalikuwa bado hayajafika nchini Kenya, ilimlazimu kuficha hali yake ya Afya hadi alipojifungua mwaka wa 1999, ila bahati mbaya mwanawe alifariki miezi miwili baadaye.

Margaret Lavonga,mwenye umri wa miaka 55 na mama wa watoto wawili, ameishi na virusi vya HIV kwa zaidi ya miaka 30.

"Nilijua niko na virusi nikiwa mjamzito baada ya kufanya vipimo na nikaambiwa matokeo yangu si mazuri"

Kipindi hicho kuugua au kupatikana na virusi vya HIV ilikuwa jambo baya kutokea kutokana na unyanyapaa uliokuja na ugonjwa huo.

"Ni wakati ambao walikuwa wameeka mabango kila mahali yakiwa na magofu ya watu ya kionyesha kichwa na mifupa.

Nilipoambiwa kwamba niko na virusi, niliona kwamba mimi nakufa kesho yake."

Kipindi hicho Margret anapatikana na virusi vya HIV, madawa ya kupunguza makali ya ugonjwa wa ukimwi yalikuwa bado hayajafika nchini Kenya, ilimlazimu kuficha hali yake ya Afya hadi alipojifungua mwaka wa 1999, ila bahati mbaya mwanawe alifariki miezi miwili baadaye.

"Hospitalini kujifungua hali ilikuwa ngumu, kila mtu aliogopa kunikaribia wakihofia kuambukizwa ukimwi"

Baada ya hapo Margaret akaanza kuugua, kwa muda wa miaka miwili, hangeweza kutoka kitandani, akihudumiwa na dadake ambaye alikuwa anaelewa hali yake wakati huo.

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Alilazwa hospitalini mara kadhaa, bahati nzuri alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kupata madawa ya kupunguza makali ya ukimwi nchini Kenya.

Kisa cha kwanza cha HIV kiliripotiwa nchini Kenya mwaka wa 1984, na kwa wale walioapatikana na ugonjwa huo wakati huo, siku zao za kuishi zilikuwa zinahesabiwa.

Wengi walikumbana na unyanyapaa, kutengwa na familia na marafiki, huku watoto wengi wakisalia mayatima.

Ila kuna wale kama Margaret waliopata virusi vya HIV miaka mwaka wa 1999, wameishi nao kwa zaidi ya miaka 30 na sasa wanazeeka wakiwa na virusi hivyo.

Kwake safari ya kumeza dawa za kupunguza makali ya ukimwi ARV's haijakuwa rahisi.

"Mwanzoni tulikuwa tunapewa dawa tatu tofauti,hizo dawa zilikuwa kubwa, zilikuwa na madhara mengi, wakati mwingine ungemeza dawa hizo ungepata ndoto au njozi haujihisi ukiwa wewe, wakati mwingine unaendesha.

Naweza sema wale wanapata virusi kwa sasa wanabahati kwasababu dawa wanazomeza hazina madhara kubwa."

Margaret anatuelezea kuwa kabla ya kuanza kumeza madawa alikuwa tayari kwa kifo kwani tayari alikuwa amepunguza uzani wa mwili wake hadi kufikia kilo 34, na wazazi wake waliposikia kuhusu hali yake wakaanza kuandaa mazishi yake.

Kuna kipindi aliacha kumeza dawa kwa madai kuwa ameokoka na kutegemea maombi, ila hali yake ya afya ikadorora tena mara moja, ikabidi akue mtiifu kwa kumeza dawa hadi sasa.

Virusi vya HIV hulenga seli nyeupe za damu, na kudhoofisha kinga ya mwili. Hii huifanya

#war

📌 Kaynak

Bu haber XML kaynağından derlenmiştir. Tamamı için orijinal habere gidin.

Orijinal haberi oku →
📱
News AI World — Mobil uygulama
Bu haberleri 45 dilde, anlık çeviriyle cebinde. Erken erişim için Gmail adresini bırak.
← Tüm haberlere dön