Kwa nini uume ni kipimo muhimu cha afya ya mwanaume
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi punde, wanaume wenye tatizo la kushindwa kusimamisha uume walibainika kuwa na uwezekano mkubwa kwa asilimia 59 wa kupata ugonjwa wa mishipa ya moyo na uwezekano mkubwa kwa asilimia 34 wa kupata kiharusi.
Tatizo la kushindwa kusimamisha uume linaweza kuwa ishara ya awali ya mshtuko wa moyo, kiharusi, kisukari na hata maradhi ya kupoteza kumbukumbu.
Watafiti wanasema ni wakati wa wagonjwa na madaktari kulichukulia suala hili kwa uzito zaidi.
Tatizo la kushindwa kusimamisha uume linaweza kuelezwa kama janga la kimya kimya.
Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa zaidi ya nusu ya wanaume wenye umri wa zaidi ya miaka 40 hukumbwa na hali hii kwa kiwango fulani. Hata hivyo, wengi wao husita kuzungumzia tatizo hilo, hata na watu wao wa karibu.
Linapojitokeza katika mazungumzo, mara nyingi suala hili huchukuliwa kama mzaha badala ya kuonekana kama ishara ya mapema ya matatizo makubwa ya kiafya yanayoweza kujitokeza baadaye. Lakini utafiti unaozidi kuongezeka unaonyesha kuwa afya ya uume inaweza kuwa kiashiria muhimu cha afya ya jumla ya mwanaume.
Wataalamu wanaeleza kuwa tatizo la kushindwa kusimamisha uume linaweza kuwa ishara ya magonjwa mbalimbali makubwa, yakiwemo kisukari, magonjwa ya moyo, kiharusi na maradhi ya mfumo wa fahamu yanayosababisha kupungua kwa uwezo wa kufikiri na kukumbuka.
Kwa mujibu wa mtaalamu wa afya ya ngono, Emmanuele Jannini wa Chuo kikuu cha Rome Tor Vergata, tatizo la kushindwa kusimamisha uume ni kama "kengele ya tahadhari ya mapema" inayoweza kuashiria kuwepo kwa matatizo makubwa ya kiafya mwilini. Jannini, ambaye hivi karibuni alihariri kitabu cha kitaaluma kinachochambua ushahidi uliopo kuhusu suala hili, anasema kuwa uchunguzi wa mapema na wa kina wa tatizo hilo unaweza kuwasaidia madaktari kubaini magonjwa hatari yanayowakabili wanaume kabla hayajafikia hatua mbaya.
Hata hivyo, wanaume wengi husita kuzungumzia afya yao ya kingono kutokana na aibu au hofu, hali inayowafanya kukosa fursa muhimu za kugundua na kutibu matatizo ya kiafya mapema.
Haya ndiyo unayohitaji kujua kuhusu dalili na ni wakati gani unapaswa kumuona daktari.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Kama ilivyo kwa magonjwa mengi, kiwango halisi cha kuenea kwa tatizo la kushindwa kusimamisha uume hutegemea namna linavyofafanuliwa na kupimwa. Kwa sababu hiyo, tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa kiwango chake duniani miongoni mwa wanaume watu wazima kinatofautiana kutoka asilimia 3 hadi asilimia 76.5, tofauti kubwa sana.
Hata hivyo, mojawapo ya tafiti kubwa na za kina zaidi iliwahusisha takribani watu 1,200 kwa kutumia dodoso za kina na kubaini kuwa asilimia 39 ya wanaume wenye umri wa miaka 40 walikumbwa mara kwa mara na kiwango fulani cha udhaifu wa nguvu za kiume. Kiwango hicho kiliongezeka hadi asilimia 67 kwa wanaume w
📌 Kaynak
Bu haber XML kaynağından derlenmiştir. Tamamı için orijinal habere gidin.
Orijinal haberi oku →