Iran yasema imeshinda vita, wananchi wake wanauonaje ushindi huo?
Ila kuna raia wa Iran ambao wapo ndani na nje ya nchi hiyo ambao hawaoni kama diplomasia ndiyo itatatua mgogoro uliopo, ila kwao ni nafasi nzuri ya kubadilisha utawala wa Iran.
Uongozi wa Iran umekuwa ukipendekeza makubaliano na Marekani kama ushindi kutokana na ustahimilivu wao ila hoja hiyo si rahisi kukubalika haswa na raia wa Iran.
Taifa hilo limepitia wakati mgumu, uchumi wao umeathirika pakubwa huku wanaounga mkono Iran wakikanusha kila siku kuwa hawatalegeza Kamba ikija katika matakwa yao na Washington.
Ila kuna raia wa Iran ambao wapo ndani na nje ya nchi hiyo ambao hawaoni kama diplomasia ndiyo itatatua mgogoro uliopo, ila kwao ni nafasi nzuri ya kubadilisha utawala wa Iran.
Maafisa wakuu wa Israel wametangaza makubaliano na Marekani kama ushindi. Mohammed Bagher Qalibaf, spika wa bunge la Iran alisema "Iran imechukua hatua ndefu kufikia ushindi huu"
Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian amesema makubaliano hayo yataleta mageuzi, na iwapo yatatekelezwa kikamilifu, yatatatua matatizo mengi ya Iran yaliyoletwa na 'watu tofauti' nchini humo na Mashariki ya kati.
Semi za Qalibaf zina uzito, kwani inaonyesha kuwa makubaliano na Marekani yanaungwa mkono na viongozi wengine wakuu wa Iran ikiwemo jeshi la IRGC.
Uongozi wa Iran pia unatangaza makubaliano hayo kuwa ushindi kwani Marekani na Israel wameshindwa kuafikia malengo yao katika vita walivyoanzisha nchini Iran.
Walishindwa kuishinikiza Iran kujisalimisha, walishindwa kubadilisha mfumo wa uongozi wa kiislamu, na hawakuweza kumaliza mpango wa nyuklia wa Iran kupitia nguvu za kijeshi, na pia hawakuvunja uhusiano wa Iran na Hezbollah.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Licha ya yote, Iran bado ina uwezo wa kufanya majadiliano, huku Lebanon ikijumuishwa katika makubaliano yao ya kupatikana kwa amani.
Ila simulizi ya Iran kuwa imeshinda vita, inapokea changamoto ndani ya Iran.
Mbunge mmoja mwenye msimamo mkali nchini Iran, amesema makubaliano hayo yataigeuza Iran kuwa chini ya utawala wa Marekani. Pia aliwashtumu wapatanishi wa Iran kwa kuenda kinyume na agizo la kiongozi mkuu wa kutofungua Mlango Bahari wa Hormuz.
Ukosoaji huo una uzito kwani unatoka ndani ya utawala wa Iran.
Kwa miezi kadhaa, viongozi tofauti, vyombo vya habari wamekuwa wakisisitiza kuwa Marekani si taifa ya kuaminiwa.
Kulingana na Iran, vita vilianza wakati mazungumzo yanaendelea, na kuishtumu Marekani kwa kutumia kipindi cha mazungumzo kujiandaa kwa vita Pamoja na Israel.
Makubaliano na Marekani awali yalipokea pingamizi nyingi, ila kwa sasa, sauti za ukosoaji zimepungua, kumaamisha makubaliano hayo yameidhinishwa na ngazi ya juu ya uongozi wa taifa hilo.
Kwa sasa huenda uongozi wa taifa hilo umetathmini kuwa kukataa makubaliano hayo utakuwa na athari kub
📌 Kaynak
Bu haber XML kaynağından derlenmiştir. Tamamı için orijinal habere gidin.
Orijinal haberi oku →