Utata wa $300 bilioni za Iran unavyoibua vita mpya Marekani
Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na Reuters, mfumo wa makubaliano kati ya Washington na Tehran unajumuisha mpango wa kuanzisha mfuko wa uwekezaji wa sekta binafsi wenye thamani ya dola bilioni 300 kwa ajili ya kuchochea uwekezaji nchini Iran baada ya vita vya miezi kadhaa vilivyoikumba nchi hiyo.
Makubaliano mapya yanayojadiliwa kati ya Marekani na Iran yameanza kuzua mjadala mkali ndani ya siasa za Marekani, huku mfuko wa uwekezaji wenye thamani ya dola bilioni 300 ukiwa kiini cha mabishano yanayoweza kumletea Rais Donald Trump changamoto kutoka kwa wafuasi wake mwenyewe.
Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na Reuters, mfumo wa makubaliano kati ya Washington na Tehran unajumuisha mpango wa kuanzisha mfuko wa uwekezaji wa sekta binafsi wenye thamani ya dola bilioni 300 kwa ajili ya kuchochea uwekezaji nchini Iran baada ya vita vya miezi kadhaa vilivyoikumba nchi hiyo.
Ingawa maafisa wa Marekani wanasisitiza kuwa fedha hizo hazitatoka kwa walipa kodi wa Marekani, na kwamba zitachangiwa na wawekezaji kutoka nchi za Ghuba, Asia, Afrika na maeneo mengine duniani, hoja hiyo haijatosha kuwanyamazisha wakosoaji wa makubaliano hayo.
Kwa miaka mingi, Trump alikuwa mkosoaji mkubwa wa makubaliano ya nyuklia ya Iran yaliyofikiwa mwaka 2015 chini ya Rais Barack Obama. Mara kwa mara aliwashutumu viongozi wa wakati huo kwa "kuipa Iran mamia ya mabilioni ya dola" na kudai fedha hizo zingetumika kufadhili ugaidi duniani.
Katika mikutano ya kampeni, mijadala ya urais na mahojiano mbalimbali, Trump aliitaja mara kwa mara takwimu ya dola bilioni 150 ambazo Iran iliruhusiwa kuzifikia kupitia mali zake zilizokuwa zimezuiwa chini ya vikwazo vya kimataifa.
Sasa, wapinzani wake wanahoji tofauti iliyopo kati ya msimamo huo wa zamani na makubaliano ya sasa ambayo yanaweza kuipa Iran fursa ya kufaidika na mfuko wenye thamani mara mbili ya kiasi hicho.
Makamu wa Rais JD Vance alizidisha mjadala huo baada ya kueleza kuwa Iran inaweza kupata fursa ya kunufaika na mfuko huo iwapo itatekeleza masharti ya makubaliano mapya, ikiwemo kusitisha shughuli zinazohusiana na mpango wake wa nyuklia na kukubali mfumo mkali wa ukaguzi.
Baada ya kauli hiyo, Ikulu ya White House ilijikuta ikitoa maelezo ya ziada ikisisitiza kuwa si Marekani inayotoa fedha hizo bali wawekezaji wa kimataifa na washirika wa kikanda.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Hata hivyo, kwa wakosoaji wengi wa Trump ndani ya mrengo wa kihafidhina, hoja kuu si chanzo cha fedha hizo bali matokeo yake. Wanasema kuwa kuifungulia Iran njia ya kupata mtaji mkubwa wa kimataifa kunaweza kuipa serikali ya Tehran afueni kubwa ya kiuchumi ambayo hapo awali Trump mwenyewe aliikosoa alipokuwa akishambulia makubaliano ya Obama.
Ndani ya mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya kihafidhina, baadhi ya wafuasi wa Trump tayari wameanza kuuliza swali moja: ikiwa dola bilioni 150 zil
📌 Kaynak
Bu haber XML kaynağından derlenmiştir. Tamamı için orijinal habere gidin.
Orijinal haberi oku →