Kombe la Dunia 2026: Ureno v DRC - Ronaldo kuchezeshwa ndombolo?

📌 Diğer 📰 Kenya 🕐 2 saat önce
Kombe la Dunia 2026: Ureno v DRC - Ronaldo kuchezeshwa ndombolo?

Wawakilishi wa Afrika DRC wanakipiga na Ureno saa mbili kamili usiku huu. Ni vory Coast pekee kutoka Afrika aliyeanza na ushindi. Afrika Kusini, Tunisia, Senegal, Algeria zilianza kwa kipigo wakati Morocco, Cape Verde na Misri zenyewe zilianza kwa sare.

Portugal inaanza kampeni yake ya Kombe la Dunia 2026 kwa mchezo muhimu wa Kundi K dhidi ya DR Congo leo katika Uwanja wa NRG, Houston, Marekani.

Ureno inaingia ikiwa moja ya timu zinazopewa nafasi kubwa kutokana na kikosi chake chenye nyota kama Cristiano Ronaldo, Bruno Fernandes na Bernardo Silva. Chini ya kocha Roberto Martínez, Ureno inalenga kuanza kwa ushindi katika kundi ambalo pia lina Colombia na Uzbekistan.

Kwa upande wa DR Congo, wanarejea kwenye Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1974, jambo linalowapa hamasa kubwa ya kufanya vizuri.

Timu hiyo ya kocha Sébastien Desabre imejijengea sifa kwa uimara wa safu ya ulinzi na mashambulizi ya kushtukiza, huku ikiongozwa na wachezaji kama Chancel Mbemba.

Ingawa Ureno inaonekana kuwa na ubora mkubwa kwenye karatasi, mechi za Kombe la Dunia mara nyingi huleta matokeo ya kushangaza, hivyo DR Congo itajaribu kupambana kwa nguvu ili kuanza safari yake kwa matokeo mazuri.

📌 Kaynak

Bu haber XML kaynağından derlenmiştir. Tamamı için orijinal habere gidin.

Orijinal haberi oku →
📱
News AI World — Mobil uygulama
Bu haberleri 45 dilde, anlık çeviriyle cebinde. Erken erişim için Gmail adresini bırak.
← Tüm haberlere dön