Kombe la Dunia 2026: DRC yaendelea kuivimbia Ureno
Wawakilishi wa Afrika DRC wanakipiga na Ureno saa mbili kamili usiku huu. Ni vory Coast pekee kutoka Afrika aliyeanza na ushindi. Afrika Kusini, Tunisia, Senegal, Algeria zilianza kwa kipigo wakati Morocco, Cape Verde na Misri zenyewe zilianza kwa sare.
Chris Sutton Fowadi wa zamani wa Uingereza kwenye BBC Radio 5 Live katika Uwanja wa Houston Ureno
Hawajaonyesha nia ya kutosha na kadiri muda ulivyoendelea DR Congo walianza kutamani bao hili.
Lo! Yoane Wissa aifungia DR Congo bao la kwanza kabisa kwenye Kombe la Dunia.
Ureno wanaudhibiti kabisa mpira, lakini wanaupiga kutoka upande hadi upande kwa sasa.
Joao Neves anakimbia nyuma ya safu ya ulinzi ya DR Congo, lakini mpira wa Pedro Neto unakatwa haraka. hatari inaondolewa!
Wimbi la Mexican linazunguka katika Uwanja wa Houston. Kwa kweli kufikia sasa haujawa mchezo wa kufurahisha
Ureno haijajaribu hata shuti moja katika dakika 30 zilizopita
Pedro Neto yuko chini akishika koo lake baada ya kuvutwa shati na Chancel Mbemba.
Ureno wamedhibiti kwa kiasi kikubwa mchezo. Wanajua lini wapunguze kasi ya mambo kupitia Vitinha na Joao Neves.
"Ni mwanzo wa kutetereka na na mbaya kwa DR Congo. Joao Neves anafunga vyema umbali wa yardi 12 anapiga kichwa maridadi. Ni kichwa cha ajabu - amemalizi kwa ustadi. Mwanzo bora kwa Ureno".
Mjadala umeendelea kwa miaka mingi kuhusu kama Ureno ingenufaika zaidi bila uwepo wa Cristiano Ronaldo lakini inaonekana hakuna hatari ya karibu ya nyota huyo wa kimataifa mwenye umri wa miaka 41 kupoteza nafasi yake katika kikosi cha kwanza.
Kocha mkuu wa Ureno Roberto Martinez hapo awali amepuuza mazungumzo kuhusu Ronaldo kama "amebebwa", akionyesha rekodi ya nahodha huyo ya mabao 25 katika mechi zake 32 zilizopita. Haijalishi kwamba mengi ya mabao hayo yalitokana na timu zilizo nje ya nafasi ya 30 bora katika viwango vya Fifa.
Ronaldo ndiye mchezaji mwenye rekodi ya dunia kwa wanaume kwa mechi na mabao mengi. Kwa kiasi kikubwa, Ronaldo anapimwa kwa mabao, na amecheza mechi tisa bila bao katika mashindano makubwa.
Karibu saa 16 baada ya Lionel Messi kuwa mchezaji wa kwanza kucheza katika Kombe la Dunia sita tofauti, Cristiano Ronaldo wa Ureno atakuwa wa pili. Anaanza mbele na atakuwa mtu wa kwanza kufunga katika fainali sita tofauti za Kombe la Dunia ikiwa atafunga bao.
Beki wa Manchester City Ruben Dias hayupo kutokana na jeraha lakini mchezaji mwenzake wa zamani wa City Bernardo Silva, winga wa Chelsea Pedro Neto na nahodha wa Manchester United Bruno Fernandes wanaanza.
Beki wa kulia wa West Ham Aaron Wan-Bissaka na mshambuliaji wa Newcastle Yoane Wissa ni miongoni mwa wachezaji wanaocheza England waliotajwa katika kikosi cha kuanza cha DR Congo.
Axel Tuanzebe, ambaye alichezea Burnley msimu uliopita katika Ligi kuu ya England , ni sehemu ya ulinzi wa mabeki watano, huku mchezaji wa Watford Edo Kayembe akianza katikati ya
📌 Kaynak
Bu haber XML kaynağından derlenmiştir. Tamamı için orijinal habere gidin.
Orijinal haberi oku →