Tetesi za usajili: Man Utd na Spurs 'zatoana roho' kwa Summerville
Manchester United na Tottenham zamuwania Summerville, Chelsea yamfuatilia Diogo Costa huku Cambiaso naye akiwa kwenye rada zao
Manchester United na Tottenham Hotspur zimeanza harakati za kumsajili mshambuliaji wa Uholanzi, Crysencio Summerville, mwenye umri wa miaka 24, kutoka West Ham United. (Teamtalk)
Chelsea inaendelea kumfuatilia kipa wa Porto na timu ya taifa ya Ureno, Diogo Costa, mwenye umri wa miaka 26, huku ikitafakari uwezekano wa kuwasilisha ofa ya pauni milioni 51 kwa ajili ya huduma zake.(Mirror)
Vilevile, Chelsea inamuwania beki wa pembeni wa Italia, Andrea Cambiaso, mwenye umri wa miaka 26, kutoka Juventus. Klabu hiyo inaweza kumjumuisha mshambuliaji wa Senegal, Nicolas Jackson, mwenye miaka 24, katika makubaliano hayo.(Gazzetta dello Sport - in Italian)
Ripoti zinaeleza kuwa madai ya Real Madrid kuwasilisha ofa kwa mshambuliaji wa Argentina wa Atletico Madrid, Julian Alvarez, mwenye umri wa miaka 26, hayakuwa ya kweli. Badala yake, kiungo mshambuliaji wa Bayern Munich na Ufaransa, Michael Olise, mwenye miaka 24, ndiye anayesalia kuwa lengo kuu la mabingwa hao wa Hispania. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Manchester United haina mpango wa kufanya mazungumzo mapya na Barcelona kuhusu mkataba mwingine wa mkopo kwa mshambuliaji wa England, Marcus Rashford, mwenye umri wa miaka 28. (ESPN)
Tottenham imekataa ofa ya pili kutoka Brighton yenye thamani ya pauni milioni 35 kwa ajili ya beki wa kati wa Croatia, Luka Vuskovic, mwenye miaka 19, ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo katika klabu ya Hamburg. (Teamtalk)
Spurs pia imeanza mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ujerumani chini ya miaka 21, Said El Mala, mwenye umri wa miaka 19, kutoka Cologne. Klabu hiyo inatumaini kuzishinda Newcastle United na Nottingham Forest katika mbio za kupata saini yake.
Lazio ya Italia na Feyenoord ya Uholanzi zinafuatilia kwa karibu mustakabali wa kiungo wa England mwenye miaka 20, Charlie Gray, wa Manchester City.(Football Insider)
Nchini Marekani, Gotham FC imefikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Australia, Sam Kerr, mwenye umri wa miaka 32, ambaye kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kuondoka Chelsea ya Ligi Kuu ya Wanawake nchini England. (ESPN)
📌 Kaynak
Bu haber XML kaynağından derlenmiştir. Tamamı için orijinal habere gidin.
Orijinal haberi oku →