'Tunahofia maisha yetu': Muda wa mwisho kwa wahamiaji kuondoka Afrika Kusini wakaribia
Waandamanaji wameweka tarehe 30 Juni kuwa siku ya mwisho kwa wahamiaji wote wasio na nyaraka halali kuondoka nchini.
Afrika Kusini imekuwa mahali penye mazingira magumu kwa wahamiaji wasio na nyaraka halali, huku tarehe ya mwisho iliyowekwa na waandamanaji kwao kuondoka nchini ikikaribia.
"Nina hofu kubwa na nimeathirika kisaikolojia," alisema Esnat Joseph, mwanamke wa miaka 36 kutoka Malawi, alipokuwa akijaribu kuwabembeleza watoto wake watatu wa mwaka mmoja waliokuwa wakilia.
Alikimbia nyumba yake katika makazi yasiyo rasmi katika mji wa bandari wa Durban, katika jimbo la KwaZulu-Natal, na kutafuta hifadhi katika eneo la wazi ambapo hadi wageni 7,000, wengi wao wakiwa Wamalawi wamekusanyika na mali zao kwa wiki mbili zilizopita.
"Watu walikuja nyumbani kwangu na kuniambia: 'Lazima uondoke. Hatutaki muendelee kuishi hapa, hivyo rudi nchini kwenu.' Walikuwa 10 na walikuwa na silaha," alisema, akielezea jinsi kundi hilo la wanaume wa Afrika Kusini lilivyokuwa na mapanga na viboko.
"Walimkata mume wangu kichwani na shingoni. Walimshika shingo kana kwamba walitaka kumuua. Kwa neema ya Mungu bado yuko hai, lakini amelazwa hospitalini."
Watu wengi wengine walioko katika eneo hilo, ambapo mashirika ya misaada yamekuwa yakigawa mablanketi na chakula, wameripoti vitisho vya aina hiyo vya kwenda nyumba kwa nyumba.
Hali hiyo inafuatia maandamano kadhaa yaliyofanyika mwaka huu, mengi yakiwa ya amani, yaliyoongozwa na kundi la kupinga wahamiaji la March and March, chama cha upinzani ActionSA na makundi mengine, ambayo yameweka tarehe 30 Juni kuwa mwisho kwa wahamiaji wasio na nyaraka kuondoka nchini.
Wakiwa na fimbo mikononi, waandamanaji wamekuwa wakiimba "Mabahambe" , msemo wa Kizulu unaomaanisha "Waondoke."
Wakati siku ya mwisho ikiendelea kukaribia, Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, alionya siku ya Jumanne kwamba "kuwalaumu watu walio katika mazingira magumu" si suluhisho la changamoto ngumu za kiuchumi zinazoikabili nchi hiyo.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Esnat Joseph alifika Afrika Kusini miaka mitatu iliyopita na alikuwa akifanya kazi ya ndani kabla ya kupata watoto wake.
Hali yake ya kisheria haijulikani wazi. Anasema alipoteza pasipoti yake na nyaraka nyingine muhimu katika tukio la wizi. Ana mpango wa kurejea Malawi kupitia mojawapo ya mabasi ambayo ubalozi mdogo wa Malawi umekuwa ukiandaa, kwa msaada wa michango, ili kuwasaidia raia wake waliokata tamaa kuondoka Durban.
Nchi za Ghana, Msumbiji, Nigeria na Zimbabwe pia zimekuwa zikiandaa safari za kurejesha raia wao kwa ndege au mabasi katika wiki za hivi karibuni, huku takribani wageni 3,500 wakijitolea kuondoka hadi sasa.
Mamlaka za Afrika Kusini zilise
📌 Kaynak
Bu haber XML kaynağından derlenmiştir. Tamamı için orijinal habere gidin.
Orijinal haberi oku →