Enzi ya mizinga inafikia mwisho, Ukraine inataka kuirudisha vipi kwenye uwanja wa vita?
Uongozi wa Jeshi la Ukraine una azma ya kubadili hali hii ya kile kinachoitwa "udhaifu wa mizinga" katika siku za usoni.
Mizinga na magari ya kivita yenye silaha nzito yanapoteza umuhimu wake kwa kasi katika uwanja wa vita kati ya Urusi na Ukraine. Hii inatokana na kuenea kwa matumizi ya droni za bei nafuu lakini zenye ufanisi mkubwa, hasa zile zinazotumia nyaya za nyuzi-optiki (fiber-optic drones), ambazo zinazuia magari hayo kufika mstari wa mbele wa mapigano.
Hata hivyo, uongozi wa Jeshi la Ukraine una azma ya kubadili hali hii ya kile kinachoitwa "udhaifu wa mizinga" katika siku za usoni.
Migogoro ya kisasa ya kijeshi duniani inazidi kugeuka kuwa "vita vya droni." Droni hizi, ambazo ni za gharama nafuu na zenye ufanisi mkubwa, zinaifanya silaha nzito na ghali kama mizinga na magari ya kivita kuwekwa pembeni katika operesheni za kivita.
Baadhi ya wataalamu wa masuala ya kijeshi hata wanazungumzia "mwisho wa enzi ya mizinga," wakisisitiza kwamba mizinga ni silaha za vita vya zamani na kwamba katika migogoro ya kisasa imeanza kubadilika kutoka kuwa faida ya kijeshi hadi kuwa mzigo na hatari kwa majeshi yanayoitumia.
Hata hivyo, mtazamo huu haukubaliwi na majenerali wa Ukraine, ambao wanaamini kuwa mizinga bado ina nafasi muhimu katika vita vya kisasa ikiwa itabadilishwa mbinu za matumizi yake na kuunganishwa na teknolojia mpya za kivita.
Zaidi ya miaka minne ya vita nchini Ukraine imepunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya mizinga na magari ya kivita kwa pande zote mbili.
Kwa mfano, makadirio ya Makao Makuu ya Jeshi la Ukraine yanaonesha kwamba hadi tarehe 3 Juni, Urusi ilikuwa imepoteza karibu magari ya kivita 37,000. Haya yanajumuisha takribani mizinga 12,000 na magari ya kivita ya mapigano 24,700.
Kwa upande mwingine, kulingana na makadirio ya mradi wa kimataifa wa uchambuzi wa kijeshi Oryx, Ukraine imepoteza karibu magari ya kivita 6,000 tangu vita vilipoanza, ambapo takribani 1,400 kati yake ni mizinga.
Hasara hizi kubwa zinaonesha jinsi vita vya kisasa, vinavyotawaliwa kwa kiasi kikubwa na droni, makombora ya kisasa na mifumo ya upelelezi wa hali ya juu, vilivyoongeza hatari kwa matumizi ya mizinga na magari ya kivita kwenye uwanja wa mapambano.
Hizi ni takwimu kubwa sana, zikiwa mara nyingi zaidi ya idadi yote ya mizinga na magari ya kivita inayomilikiwa na baadhi ya mataifa makubwa ya Ulaya kama Ufaransa na .Ujerumani.
Kwa sasa, ili kujilinda dhidi ya mashambulizi ya droni, majeshi ya Urusi na Ukraine yamelazimika kufunika mizinga na magari yao ya kivita kwa miundo mikubwa ya chuma inayojulikana kama "braziers" (au vizimba vya kinga).
Muundo wa chuma huwekwa juu na kuzunguka magari ya kivita ili kupunguza uwezekano wa kushambuliwa na droni zinazoruka juu na
📌 Kaynak
Bu haber XML kaynağından derlenmiştir. Tamamı için orijinal habere gidin.
Orijinal haberi oku →