Tetesi za Soka: Ofa ya kwanza ya Arsenal kwa Monga 'yapigwa chini'
Ofa ya kwanza ya Arsenal kwa Jeremy Monga imekataliwa na Leicester, Gunners pia wanajiandaa kumsaka Bradley Barcola na RB Leipzig wanawasiliana na Everton juu ya Barry.
Ofa ya kwanza ya Arsenal kwa Jeremy Monga imekataliwa na Leicester, Gunners pia wanajiandaa kumsaka Bradley Barcola na RB Leipzig wanawasiliana na Everton juu ya Barry.
Ofa ya kwanza ya Arsenal kwa winga wa Leicester City na Uingereza chini ya umri wa miaka 19 Jeremy Monga imekataliwa. Mchezaji huyo ni mmoja wa wale ambao wamewindwa kwa muda mrefu na klabu hiyo msimu huu. (Telegraph - subscription required)
Gunners pia wanajiandaa kumsaka winga wa Paris St-Germain na Ufaransa Bradley Barcola, 23. (Independent)
RB Leipzig wamewasiliana na Everton juu ya mshambuliaji wa Ufaransa wa chini ya miaka 21 Thierno Barry. (Times - subscription required)
Timu ya Toffees bado haijapokea ofa rasmi kwa ajili ya Barry, lakini ikiwa ofa itatolewa na timu ya RB Leipzig ya Ujerumani au klabu nyingine yoyote, kundi la uongozi wa soka la Everton litaamua jinsi ya kuendelea. (Liverpool Echo)
Real Madrid wanatafuta kuendelea kujiimarisha kwa kusajili kiungo wa kati na beki wa kati, huku kiungo wa kati wa Chelsea na Argentina Enzo Fernandez, 25, akiwa mmoja wa wale wanaochukuliwa kuwa na mchezo wa juu na klabu hiyo. (ESPN)
Tottenham wako kwenye kinyang'anyiro kikali cha kumsajili kiungo wa Anderlecht na Ubelgiji Nathan De Cat, 17 huku Manchester United ikiwa mmoja wao kutoka Ligi Kuu. (Teamtalk)
Liverpool wamefufua nia yao ya kumsajili kiungo wa kati wa Juventus na Ufaransa Khephren Thuram mwenye umri wa miaka 25. (Corriere dello Sport via Football Talk)
Liverpool pia wamemsajili winga wa Uhispania Victor Munoz - na aliiambia RB Leipzig kwamba watalipa kitita cha takriban euro 100m (£86m) kwa ajili ya Yan Diomande.
Reds walithibitisha kumsajili Munoz kutoka Osasuna baada ya kufaulu kwa juhudi zao za kushawishi kutekelezwa kwa kifungu chake cha kuuzwa kwa euro 40m (£34.5m. (Football Insider)
📌 Kaynak
Bu haber XML kaynağından derlenmiştir. Tamamı için orijinal habere gidin.
Orijinal haberi oku →