Saba saba: Watu 10 wakamatwa Jijini Nairobi huku Tanzania ikichukua tahadhari kukabiliana na tishio la maandamano
Hali ya ulinzi imeonekana kuimarishwa zaidi katika jiji kuu la kibiashara la Tanzania Dar es Salaam, huku mamia ya maafisa polisi na jeshi wakionekana kutanda katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo.
Hali ya ulinzi imeonekana kuimarishwa zaidi katika jiji kuu la kibiashara la Tanzania Dar es Salaam, huku mamia ya maafisa polisi na jeshi wakionekana kutanda katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo.
Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Nairobi, Issa Mohamud, amesema kuwa maandamano ya Saba Saba ya mwaka huu katika jiji la Nairobi yalikuwa ya amani kwa kiwango kikubwa, huku watu 10 pekee wakikamatwa wakati polisi wakidumisha sheria na utulivu siku nzima.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya maandamano hayo, Mohamud alisema washukiwa sita walikamatwa katika eneo la Pangani.
"Namna wananchi walivyojiendesha leo imethibitisha tena kwamba Kenya ni taifa linaloongozwa na utaratibu, umoja na kuheshimiana. Tumewakamata watu 10 pekee—sita katika eneo la Pangani na wanne ndani ya eneo la Kituo cha Polisi cha Central," alisema Mohamud.
Aliwapongeza wananchi kwa kujizuia na kudumisha amani wakati wa maandamano hayo, akibainisha kuwa mwenendo wa amani wa waandamanaji wengi uliwezesha biashara katika maeneo mengi ya jiji kuendelea na shughuli za kawaida.
"Kwa jinsi mnavyoona, takribani asilimia 80 ya biashara ziliendelea kuwa wazi hadi wakati huu," alisema.
Kamanda huyo wa Polisi wa Kanda alisisitiza kuwa Katiba inamhakikishia kila Mkenya haki ya kukusanyika, kuandamana na kufanya maandamano ya amani, lakini akasisitiza kwamba haki hizo lazima zitumike kwa kuzingatia mipaka ya sheria.
Mohamud aliongeza kuwa inasikitisha kwamba kulikuwa na vizuizi barabarani na kusisitiza ulazima wa kukagua kwa kina wanaoingia jijini kwa ajili ya kudumisha usalama.
Wakati huo huo Jeshi la Polisi nchini Tanzania limetoa taarifa inayoeleza kuwa hali ni shwari katika nchi hiyo hadi tarehe 7 Julai, 2026 huku watu wanaendelea na shughuli zao za kiuchumi na kijamii, licha ya uwepo mkubwa wa vikosi vya usalama katika barara na mitaa.
Siku ya Saba saba: Hali ilivyokuwa jijini Nairobi kupitia picha
Duke wa Sussex Mwanamfalme Harry na watu wengine sita wameshindwa kesi yao kuhusu faragha katika Mahakama Kuu dhidi ya kampuni inayochapisha magazeti ya Daily Mail na Mail on Sunday
Kundi hilo, ambalo linajumuisha Sir Elton John, Baroness Lawrence na Liz Hurley, liliishtaki kampuni ya Associated Newspapers Limited (ANL) kwa madai ya kukusanya taarifa kinyume cha sheria.
Katika uamuzi wake, Jaji Nicklin amesema madai hayo ni mazito na yanahitaji ushahidi zaidi wa kushawishi kabla ya kuthibitishwa - lakini walalamikaji walishindwa kuyathibitisha.
Kesi ya wiki moja ilishuhudia Mwanamfalme Harry akitoa ushahidi kuhusu makala alizozilalamikia akisema kampuni hiyo imefanya maisha ya mkewe kuwa
📌 Kaynak
Bu haber XML kaynağından derlenmiştir. Tamamı için orijinal habere gidin.
Orijinal haberi oku →