Kombe la Dunia 2026: 'Anazunguka uwanjani kama mzee': Ronaldo akosolewa baada ya Ureno kuondolewa
Ronaldo alibubujikwa na machozi wakati safari yake ya Kombe la Dunia ilipofikia tamati, kufuatia bao la ushindi lililofungwa na Mikel Merino katika muda wa nyongeza.
Mmoja wa magwiji wakubwa wa soka atahitimisha taaluma yake bila kushinda taji muhimu zaidi, baada ya mechi ya mwisho ya Kombe la Dunia ya Cristiano Ronaldo akiwa na Ureno kumalizika kwa kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Uhispania katika hatua ya 16 bora.
Mchezaji huyo alibubujikwa na machozi wakati safari yake ya Kombe la Dunia ilipofikia tamati, kufuatia bao la ushindi lililofungwa na Mikel Merino katika muda wa nyongeza, bao lililoiwezesha timu ya nchi jirani kusonga mbele.
Akiwa na umri wa miaka 41, mchezaji huyo ambaye ameshinda tuzo ya Ballon d'Or mara tano, Ligi ya Mabingwa mara tano na Kombe la Mataifa ya Ulaya (Euro) mwaka 2016, amefunga mabao 976 —rekodi ya dunia— akiwa na klabu zake pamoja na timu ya taifa.
Amefunga mabao katika mashindano sita ya Kombe la Dunia, rekodi ya kihistoria.
Hata hivyo, hatua ya karibu zaidi aliyofikia katika mbio zake a kushinda Kombe la Dunia ilikuwa mwaka 2006, wakati Ureno ilipotinga nusu fainali.
Tayari alikuwa ametangaza kuwa hili lingekuwa Kombe lake la Dunia la mwisho, lakini baada ya mechi hiyo alisema: "Nitajadiliana na familia yangu na kufanya maamuzi kwa utulivu," alipoulizwa iwapo ataendelea kuichezea timu yake ya taifa.
Mjadala utaendelea kuwa wazi laitiUreno wangekuwa na nafasi nzuri zaidi ya kushinda Kombe hili la Dunia bila shinikizo la kumwanzisha Ronaldo - mchezaji wa klabu ya Al-Nassr - katika kila mechi.
Hata hivyo, kwa mchambuzi wa BBC Chris Sutton, ambaye alikuwa kwenye mchezo huo mjini Dallas, hakukuwa na shaka.
"Anazunguka uwanja kwa shida, kama mzee; ndiyo maana Ureno haipo," alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa Uingereza.
"Roberto Martínez anafanya nini? Unawezaje kumfurahisha mchezaji kiasi hiki?"
Kocha Martinez alitangaza kujiuzulu baada ya firimbi ya mwisho na kumsifu Ronaldo, ambaye alimwita "nyota wa soka".
"Tunapaswa kumshukuru kwa kile alichojaribu kufanya katika Kombe hili la Dunia," Martinez alisema.
"Ndoto yake ilikuwa kushinda Kombe hili la Dunia, na alikabiliana nayo kwa kutoa mfano wa ajabu."
"Yeye ni mfano mzuri wa kile soka inawakilisha na ubora wa binadamu kwenye ulingo wa mwanariadha."
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Suala kuu linalojirudia mara kwa mara katika mashindano makubwa ya hivi karibuni ni iwapo Ronaldo anapaswa kuwa mmoja wa wachezaji wanaoanza mechi.
Amefunga mabao 146 kwa timu yake ya taifa, rekodi katika soka la kimataifa la wanaume, lakini hivi karibuni baadhi ya watu wamehoji iwapo bado ana mchango mkubwa uwanjani.
Na, kutokana na umaarufu na hadhi yake inayovuka mipaka ya michezo, inaonekana Martinez
📌 Kaynak
Bu haber XML kaynağından derlenmiştir. Tamamı için orijinal habere gidin.
Orijinal haberi oku →