Tunafanya mazungumzo na Iran ila usitishaji mapigano umefutiliwa mbali - Trump
Kauli hiyo imekuja baada ya Marekani kushambulia maeneo kadhaa katika majimbo matano kusini mwa Iran kufuatia mashambulizi dhidi ya meli zilizokuwa zikipita eneo hilo.
Kauli hiyo imekuja baada ya Marekani kushambulia maeneo kadhaa katika majimbo matano kusini mwa Iran kufuatia mashambulizi dhidi ya meli zilizokuwa zikipita eneo hilo.
Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa Marekani inaendelea kufanya mazungumzo na Iran lakini amesisitiza kuwa usitishaji wa mapigano umefutiliwa mbali.
Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mitandao ya kijamii, Trump alisema: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetuomba kuendelea na mazungumzo. Tumekubali ombi hilo, lakini Marekani imewaeleza wazi kwamba usitishaji wa mapigano umefutwa."
Kauli hiyo imekuja baada ya Marekani kushambulia maeneo kadhaa katika majimbo matano kusini mwa Iran, kufuatia mashambulizi dhidi ya meli zilizokuwa zikipita eneo hilo.
Marekani na Iran zimetupiana lawama kwa kushindwa kudumisha makubaliano yaliyokuwa yamefikiwa.
Aidha, maafisa wa Iran wamesema nchi hiyo ina haki ya kujibu mashambulizi yoyote yanayolenga miundombinu yake.
Mambo matano yanayoifanya Iran ya sasa kuwa tofauti kabisa na ilivyokuwa awali
Makubaliano ya Marekani na Iran yaibua maswali iwapo kulikuwa na haja yoyote ya vita
Idadi ya meli za kubeba mafuta zinazopita kila siku katika Mlango Bahari wa Hormuz imeonekana kupungua hii leo siku ya Ijumaa, baada ya Marekani na Iran kushambuliana na kuendeleza mabishano kuhusu nani anayedhibiti njia hiyo muhimu ya baharini.
Mashambulizi hayo yamezua tena wasiwasi kuhusu kuimarika kwa shughuli za usambazaji wa mafuta duniani na usafirishaji kwa njia ya bahari.
Hali hii inaonyesha jinsi makubaliano ya muda ya kusitisha mapigano yalivyo dhaifu huku Marekani na Iran zikiendelea kujadiliana ili kufikia makubaliano ya kudumu.
Vyombo vya habari vya Iran vyachapisha picha la kaburi la Ali Khamenei
Vyombo vya habari vya Iran vimechapisha picha ya eneo alikozikwa aliyekuwa kiongozi mkuu wa Iran, Ali Khamenei, na jamaa zake wanne mjini Mashhad.
Khamenei aliuawa zaidi ya miezi minne iliyopita, siku ya kwanza ya mashambulizi ya Israel na Marekani dhidi ya Iran, katika ofisi yake iliyopo Mtaa wa Pasteur mjini Tehran.
Mazishi hayo hayakuhudhuriwa na Mojtaba Khamenei, mwana wa kiongozi huyo wa zamani ambaye ambaye sasa ndiye kiongozi mkuu wa Iran.
Je, sheria za Kiislamu zilifuatwa wakati wa mazishi ya Ali Khamenei?
Kuanzia Tehran hadi Najaf: Tunachojua kuhusu mazishi ya Ali Khamenei
Abiria mmoja ameripotiwa kukaribia kuvutwa nje kupitia dirisha la ndege akiwa angani katika ndege ya Ryanair.
Mashahidi waliambia vyombo vya habari vya eneo hilo kwamba mwanaume huyo, anayesemekana kuwa raia wa Serbia mwenye umri wa zaidi ya miaka 60, alining'inia nje ya dirisha
📌 Kaynak
Bu haber XML kaynağından derlenmiştir. Tamamı için orijinal habere gidin.
Orijinal haberi oku →