Mashambulizi ya makombora na 'hatari inayowakabili viongozi wa Iran'

📰 Gündem 📰 BBC Swahili 🕐 2 saat önce
Mashambulizi ya makombora na 'hatari inayowakabili viongozi wa Iran'

Siku za hivi karibuni lugha ya vita na vitisho imeonekana kushamiri katika taarifa za maafisa wa Iran kuliko kuzingatia diplomasia na ''mazungumzo".

"Tunafikia makubaliano kupitia makombora sio mazungumzo. Kwenye meza ya mazungumzo tunakuja kujadili kilichotokea. "Kauli hii ya kutisha ni mojawapo ya machapisho ya hivi punde zaidi ya mpatanishi mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mohammad Bagher Ghalibaf, kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Siku za hivi karibuni lugha ya makabiliano na vitisho imeonekana kushamiri katika taarifa za maafisa wa Iran kuliko kuzingatia diplomasia na ''mazungumzo".

Uchunguzi wa matamshi ya maafisa wa kisiasa na kijeshi unaonyesha kuwa wanazidi kusisitiza hatua za kijeshi na makabiliano. Mohsen Rezaei, kamanda wa zamani wa IRGC na mshauri wa kijeshi wa Amiri Jeshi Mkuu, pia mara kwa mara amezungumzia uwezekano wa hatua ya tahadhari ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na, kwa mujibu wa Mohammad Baqer Qalibaf: "Tutavunja kizuizi cha majini ima kwa mazungumzo au hatua ya moja kwa moja."

"Mazungumzo" ni mojawapo ya maneno yanayotumiwa mara kwa mara kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, sambamba na vita na usitishaji mapigano. Neno hilo limekuwa likitumika sana kiasi kwamba kwa baadhi ya watu limeibua neno duru nyingine ya mazungumzo kati ya Iran na mataifa ya Magharibi ambayo wakosoaji wameyataja kuwa ya matamshi yasiyo na tija.

Katika miaka iliyopita wakati Saeed Jalili alipokuwa mpatanishi mkuu wa nyuklia wa Iran chini ya Rais Mahmoud Ahmadinejad, maafisa wa Iran mara kwa mara walizungumzia kuhusu hatua zilizopigwa katika mazungumzo hayo, lakini mchakato huo wakati mwingine ulikwama na hata mara nyingine kufikia mkwamo.

Sasa, baada ya zaidi ya miongo miwili ya mazungumzo na kufuatia mizozo miwili ya kijeshi katika mwaka uliopita, majadiliano ya vita na mazungumzo yamekuwa yakizingatiwa zaidi kuliko hapo awali. Kiasi kwamba siku moja, uvumi kuhusu makubaliano na kuanza tena kwa mazungumzo yanafufuliwa, na saa kadhaa baadaye, maafisa kutoka pande zinazozozana wanazungumzia uwezekano wa ukiukaji wa makubaliano ya usitishaji mapigano, utayari wa kijeshi, na uwezekano wa mapigano kuzuka upya.

Masoko pia yanaonekana kunganyika na taarifa zinazojirudia kuhusu mazungumzo. Ingawa kauli za maafisa wakuu, akiwemo Donald Trump, bado zinaweza kuathiri soko la mafuta, thamani ya sarafu na bei ya dhahabu, kwani huathiriwa na taarifa kama vile "makubaliano yanakaribi kufikiwa". Hata hivyo, matukio yasiyotarajiwa au taarifa muhimu za maafisa wakuu bado zinaweza kusababisha mabadiliko makubwa.

Mazungumzo hayo yamekuwa na heka heka zake tangu kuafikiwa kwa makubaliano ya usitishaji vita wa wiki mbili Aprili 9. Lakini pengine muhimu zaidi kuliko mazungumzo yenyewe ni masimulizi yanayo

#diplomasi

📌 Kaynak

Bu özet BBC Swahili kaynağından otomatik derlenmiştir. Tamamı için orijinal habere gidin.

Orijinal haberi oku →
← Tüm haberlere dön