Je, ni akina nani wanaoshikilia rekodi za Kombe la Dunia?

📌 Diğer 📰 BBC Swahili 🕐 9 saat önce
Je, ni akina nani wanaoshikilia rekodi za Kombe la Dunia?

Kombe la Dunia la 2026 linalofanyika Marekani, Canada na Mexico tayari ni mchuano uliovunja rekodi.

Kombe la Dunia la 2026 linalofanyika Marekani, Canada na Mexico tayari ni mchuano uliovunja rekodi.

Likiwa na timu 48, ni Kombe la Dunia kubwa zaidi katika historia, likileta ongezeko la 50% kutoka kwa timu 32 ambazo zimeshiriki Kombe la Dunia la 1998 nchini Ufaransa.

Lakini kuna rekodi nyingi zaidi ambazo zinaweza kuvunjwa mwaka huu, ikiwa ni pamoja na dakika nyingi za kucheza, mabao mengi ya mtu binafsi na mabao mengi ya timu.

Huu hapa ni mtazamo wa baadhi ya wanaoshikilia rekodi za Kombe la Dunia kwa sasa na jinsi wanavyokaribia kuzipoteza - au kushinda .

Katika historia ya miaka 96 ya Kombe la Dunia la Fifa kwa wanaume, ni mataifa manane pekee ndiyo yameshinda mashindano hayo. Kati ya mataifa hayo manane, sita wameshinda mara nyingi.

Brazil wanashikilia rekodi ya kushinda mara nyingi zaidi Kombe la Dunia kwa mara tano, wakiibuka washindi mwaka 1958, 1962, 1970, 1994 na 2002.

Ujerumani na Italia ndiyo mataifa yanayofuata kwa mafanikio zaidi kwa kutwaa vikombe vinne kila moja. Ushindi wa marar tatu wa Ujerumani ulikuwa chini ya jina la Ujerumani Magharibi, kabla ya taifa hilo kuunganishwa na Ujerumani Mashariki kama nchi moja baada ya Kombe la Dunia la 1990.

Mabingwa watetezi Argentina wameshinda Kombe hilo mara tatu, huku Ufaransa na Uruguay wakiwa na ushindi mara mbili wa michuano hiyo kila moja.

England na Uhispania ndio washindi pekee ambao ni mabingwa mara moja.

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Mshambulizi wa zamani wa Ujerumani Miroslav Klose anashikilia rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi katika historia ya Kombe la Dunia.

Klose alifunga mara 16 katika mechi zake 24 za Kombe la Dunia, akishikilia rekodi kwa bao moja.

Mshambulizi wa zamani wa Brazil Ronaldo anashika nafasi ya pili akiwa amefunga mabao 15 katika mechi 19 alizocheza. Gerd Muller, ambaye maisha yake ya kimataifa aliiwakilisha Ujerumani Magharibi, anashika nafasi ya tatu akiwa na mabao 14 ya Kombe la Dunia katika mechi 13 pekee.

Mshambulizi wa sasa wa Argentina Lionel Messi yuko katika nafasi ya nne pamoja na mshambuliaji wa zamani wa Ufaransa Just Fontaine. Wawili hao wana mabao 13 kila mmoja.

Mchezaji wa Real Madrid na Ufaransa Kylian Mbappe anashika nafasi ya sita. Yeye na mshindi mara tatu wa Kombe la Dunia la Brazil Pele wana mabao 12 kila mmoja.

Messi na Mbappe ndio wachezaji pekee ambao wana fursa ya kumpita Klose msimu huu wa joto.

Wawili hao walikuwa wafungaji bora kwenye Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar, wakiwa na mabao saba na nane mtawalia.

Waliotinga hatua ya tisa bora ni Sandor Kocsis (Hungary) na Jurgen Kl

📌 Kaynak

Bu özet BBC Swahili kaynağından otomatik derlenmiştir. Tamamı için orijinal habere gidin.

Orijinal haberi oku →
← Tüm haberlere dön