CCM kuna Yuda au ni homa ya urais 2030?
Mitandao ya kijamii nchini Tanzania imelipuka kwa mjadala kuhusu jina moja tu - "Yuda". Limeibuliwa na mwanasiasa Simai Mohammed Said. Yuda ni nani? Kwanini Simai ameamua kuzungumza sasa? Na kwa nini achague Bunge, badala ya vikao vya chama, kuwasilisha ujumbe huo?
Mitandao ya kijamii nchini Tanzania imelipuka kwa mjadala kuhusu jina moja tu - "Yuda". Ni jina ambalo limetamkwa mara nyingi katika siku mbili hizi, lakini bila kutajwa anayelengwa.
Aliyelirudisha jina hilo kwenye mjadala wa kitaifa ni Mbunge wa Tunguu, Zanzibar, Simai Mohammed Said. Akiwa Bungeni Dodoma wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Fedha, Simai alitoa kauli nzito kuhusu kile alichodai kuwa ni usaliti ndani ya CCM na Serikali. Akiwasilisha kwa kutumia fumbo la 'Yuda'.
Kauli hiyo ilizua maswali mengi kuliko majibu. Yuda ni nani? Kwanini Simai ameamua kuzungumza sasa? Na kwa nini achague Bunge, badala ya vikao vya chama, kuwasilisha ujumbe huo?
Lakini kadri mjadala wa "Yuda" ulivyozidi kushika kasi, swali kubwa zaidi likaanza kujitokeza. Je, Simai anazungumzia usaliti ndani ya CCM pekee, au amefungua pazia la mapambano ya urithi wa kisiasa kuelekea uchaguzi wa mwaka 2030?
Simai Mohammed Said si mwanasiasa mpya ndani ya CCM. Kabla ya kuingia kikamilifu kwenye siasa, alikuwa mfanyabiashara aliyejikita katika sekta ya utalii.
Katika safari yake ya kisiasa, amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini na ndani ya chama. Aliwahi kuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, na baadaye Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Zanzibar kabla ya kujiuzulu mwaka 2024, akieleza kuwepo kwa mazingira ambayo hayakuwa rafiki kwake kutekeleza majukumu yake.
Akiwa Bungeni, Simai alisema: "Kosa la mama ni wapi? Kwa sababu ya kumuamini mtu? Kumbe ni Yuda."
Kisha akaongeza: "Yuda huyu amesaliti ndugu zake, hata ile familia ambayo ilimlea kisiasa, hawataki kumuona huyu Yuda. Hata huko nyuma amewahi kutajwa ni mzigo, lakini leo mzigo huu tunao ndani ya Serikali."
Kwa mujibu wa Simai, mtu anayemzungumzia ameathiri wafanyabiashara, watendaji wa serikali na hata baadhi ya wanasiasa ambao safari zao za kisiasa zimekatizwa.
Lakini pamoja na uzito wa tuhuma hizo, hakumtaja mtu huyo kwa jina.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Katika simulizi za Kikristo, Yuda Iskariote anakumbukwa kwa jambo moja kuu - kumsaliti Yesu, licha ya kuwa mmoja wa wanafunzi wake wa karibu.
Ndiyo maana jina "Yuda" katika mazingira mengi ya kisiasa hutumiwa kuashiria usaliti, kutokuwa mwaminifu au kugeuka dhidi ya waliokujenga.
Simai hakufafanua moja kwa moja aliyekuwa akimlenga. Hata hivyo, kauli yake ilizua hisia kwamba ndani ya CCM kuna watu wanaoshukiwa kutokuwa waaminifu kwa misingi au historia ya chama.
Kwa wengi, muda wa kutolewa kwa kauli hiyo unaweza kuwa muhimu kuliko kauli yenyewe.
Wakati mjadala wa 'Yuda' ukiendelea, Mbunge w
📌 Kaynak
Bu özet BBC Swahili kaynağından otomatik derlenmiştir. Tamamı için orijinal habere gidin.
Orijinal haberi oku →