Kuanzia Makonda hadi Mafwele, hawa ni 'vigogo' 5 Afrika Mashariki waliopigwa marufuku kuingia Marekani

📌 Diğer 📰 BBC Swahili 🕐 26.05.2026
Kuanzia Makonda hadi Mafwele, hawa ni 'vigogo' 5 Afrika Mashariki waliopigwa marufuku kuingia Marekani

Nchi za Afrika Mashariki, zimekumbwa na vikwazo vya watu wake kuzuiwa kuingia Marekani huku majina makubwa ya kisiasa na kiusalama, kutoka Tanzania, Kenya, hadi Rwanda na Uganda yakiguswa.

Marekani imekuwa ikitumia vikwazo vya visa kama moja ya njia zake muhimu za kidiplomasia, hasa dhidi ya maafisa wa serikali na viongozi wanaotuhumiwa kwa ukiukwaji wa haki za binadamu, rushwa au kudhoofisha misingi ya demokrasia.

Hatua hizi mara nyingi hutangazwa moja kwa moja na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani na hujumuisha marufuku ya kuingia nchini humo kwa wahusika pamoja na familia zao.

Vikwazo hivi hutokana na sera inayojulikana kama Section 7031(c), ambayo hutumiwa dhidi ya maafisa wa kigeni wanaohusishwa na rushwa kubwa au ukiukwaji wa haki za binadamu.

Nchi za Afrika Mashariki, vikwazo hivi vimewahi kugusa majina makubwa ya kisiasa na kiusalama, kutoka Tanzania, Kenya, hadi Rwanda na Uganda. Wakati mwingine hatua hizi huwa za moja kwa moja na za hadharani, na wakati mwingine huwekwa kama vizuizi vya kidiplomasia visivyo na orodha ndefu ya majina.

Miongoni mwa matukio ya hivi karibuni kabisa ni hatua dhidi ya afisa wa Jeshi la Polisi Tanzania, Faustine Jackson Mafwele, ambaye ametajwa na Marekani kama mmoja wa maafisa wanaozuiwa kuingia nchini humo kutokana na madai ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Tangazo hilo limeweka jina lake kwenye orodha mpya ya watu wa Afrika Mashariki walioguswa moja kwa moja na smarufuku hiyo ya Marekani.

Faustine Mafwele ni afisa wa Jeshi la Polisi Tanzania ambaye ametajwa na Marekani mwezi Mei, 2026 kuwekwa kikwazo cha kuingia nchini humo kwa madai ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, hatua hiyo inamzuia yeye pamoja na familia yake ya karibu kuingia Marekani.

Marekani inamuhusisha Mafwele na kukamatwa kwa wanaharakani wa Kenya walioingia nchini Tanzania mwaka jana.

"Mwaka jana, jeshi la polisi liliwakamata, kuwatesa na kuwafanyia ukatili wa kingono raia wa Uganda Agather Atuhaire na raia wa Kenya Boniface Mwangi, waliokuwa jijini Dar es Salaam kufuatilia kesi mahakamani dhidi ya kiongozi wa upinzani Tundu Lissu," imeeleza sehemu ya taarifa ya Wizara hiyo ya Marekani ilisema.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Mahmoud Thabit Kombo aliiambia BBC kwamba serikali bado haijapokea rasmi taarifa ya hatua hiyo, ambayo inamzuia Mafwele kuingia nchini Marekani.

Paul Makonda, Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo alipigwa marufuku kuingia Marekani mwaka 2020 wakati huo akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

"Kwa nafasi hiyo, (Makonda) anahusishwa na ukandamizaji wa siasa za upinzani, ukandamizaji wa haki za kujieleza na kukusanyika na kulenga makundi ya wachache", ilisema taarifa ya Wizara ya mambo za Nje ya Marekani, wakati huo ikiwa chini ya Waziri

📌 Kaynak

Bu özet BBC Swahili kaynağından otomatik derlenmiştir. Tamamı için orijinal habere gidin.

Orijinal haberi oku →
← Tüm haberlere dön