Rare Earth: Je, madini haya yataleta maajabu Tanzania?
Madini muhimu ya Rare Earth Elements, yanaundwa na kundi la kemikali 17 zenye sifa za kipekee, na ni muhimu katika teknolojia mbalimbali za kisasa.
Tanzania inatarajia kukuza uchumi wake baada ya kugundulika kuwa na utajiri wa madini muhimu ya Rare Earth Elements (REEs) katika kijiji cha Mkiu, Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe, aina ya Neodymium (Nd) na Praseodymium (Pr).
Bila shaka inaeleweka kuwa Tanzania ina utajiri wa madini mengi. Uchimbaji madini hutoa zaidi ya 50% ya jumla ya mauzo ya nje ya nchi, ambayo sehemu kubwa hutokana na dhahabu. Tanzania ina akiba ya dhahabu ya wakia milioni 10.
Lakini leo hatuzungumzii dhahabu, almasi wala Tanzanite. Tunazungumzia madini muhimu ya Rare Earth Elements, ambayo yanaundwa na kundi la kemikali 17 zenye sifa za kipekee, na ni muhimu katika teknolojia mbalimbali za kisasa.
Kinachofanya madini haya kuwa ya kipekee ni sifa yake ya kuwa na sumaku, ambayo ni muhimu katika teknolojia za kila siku na nishati ya kijani.
John Mavrogenes, profesa wa jiolojia ya kiuchumi katika Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Australia, anasema, “madini haya yanaweza kutoa nishati katika uzalishaji wa umeme wa upepo, gari lako la umeme, na lifti ya ghorofa na friji.”
Ni muhimu katika utengenezaji wa mikrochip, ambazo hutumika katika kila sekta kuanzia ulinzi hadi huduma za afya. Pia hutumika katika utengenezaji wa magari ya umeme, mitambo ya kuzalisha umeme wa upepo, simu za kisasa, vifaa vya kielektroniki pamoja na teknolojia nyingine zinazotegemea nishati ya kijani.
Katika maeneo ya Ulinzi, hutumika katika mifumo ya rada, makombora ya kisasa, na miwani ya kuonea gizani. Na katika matibabu, hutumika kwenye mashine za uchunguzi wa afya na upasuaji.
Ingawa madini haya yanapatikana katika nchi nyingi, ugumu wake unatokana na kuwa membamba na huchanganyika na madini mengine. Hilo hufanya kazi ya kugundua na kuyachimba kuwa ngumu. Na mchakato wake wa kusafisha ni mgumu vilevile.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Kwa sasa China inatawala sehemu kubwa ya mnyororo wa usambazaji wa madini haya adimu duniani, ikidhibiti sehemu kubwa ya uchimbaji na kusafisha na kisha utengenezaji wa vifaa vyenye uwezo wa hali ya juu. Makampuni ya China yamezidi kupanua uwepo wao kote Afrika huku mahitaji ya kimataifa ya madini haya yakiendelea kuongezeka.
China inadhibiti karibu 70% ya uzalishaji wa madini haya duniani na ina akiba kubwa zaidi duniani. Marekani mzalishaji wa pili kwa ukubwa, huchangia takriban 13% ya uzalishaji wa kimataifa hasa kupitia mgodi wa Mountain Pass huko California.
Australia mzalishaji wa tatu kwa ukubwa duniani, huzalisha zaidi ya 7% ya ugavi wa dunia kutoka katika migodi ya mlima Weld. Nayo Myanmar inachangia takriban 5% ya uzalishaj
📌 Kaynak
Bu özet BBC Swahili kaynağından otomatik derlenmiştir. Tamamı için orijinal habere gidin.
Orijinal haberi oku →