CHADEMA vs Msajili, vita vya panzi au mgogoro wa mfumo?
Kwa takribani miaka kadhaa sasa, uhusiano kati ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa CHADEMA, umekuwa ukichukua sura ya mvutano wa mara kwa mara.
Kwa takribani miaka kadhaa sasa, uhusiano kati ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) umekuwa ukichukua sura ya mvutano wa mara kwa mara. Kila kipindi kipya cha kisiasa kinaonekana kuzaa barua mpya, onyo jipya au hatua ya kinidhamu inayolenga chama hicho kikuu cha upinzani.
Katika siku za karibuni, barua nyingine imeibuka tena, ya Mei 7, 2026, Msajili akikikitaka CHADEMA kujieleza kwa nini kisichukuliwe hatua za kisheria, ikiwemo kusimamishwa au kutozwa faini kwa madai ya ukiukaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa.
Hii si mara ya kwanza kwa hatua kama hizi kuchukuliwa dhidi ya vyama vya siasa hasa CHADEMA, jambo linalozidi kuchochea mjadala mpana kuhusu nafasi ya Msajili katika mfumo wa vyama vingi.
Wakati baadhi wakiona hatua hizi ni utekelezaji wa sheria na nidhamu ya vyama vya siasa, wengine wanaziona kama mwendelezo wa "kuandamwa kwa upinzani", hasa CHADEMA. Ndani ya mjadala huu, hoja za pande zote zimegusa masuala nyeti ambayo yamekuwa yakizunguka midomoni kila uchwao: Mamlaka ya Msajili, uhuru wa vyama, na mipaka ya usimamizi wa demokrasia.
Lakini swali kubwa linaloulizwa na wengi ni hili: Je, haya ni matukio ya kawaida ya kisheria au ni dalili za mgogoro wa kimuundo kati ya mdhibiti na wale anaowadhibiti?
Kuna uhusiano wa kipekee baina ya Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa Tanzania na vyama vya siasa, hasa vya upinzani vikiongozwa na CHADEMA.
Kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, Msajili ana jukumu la kusimamia, kuelimisha na kuhakikisha vyama vinafuata sheria. Kimsingi, ni nafasi ya "mlezi" wa mfumo wa vyama vingi.
Hata hivyo, katika vitendo, msimamo huu umeonekana kuchukua sura ya udhibiti mkali zaidi, ikijumuisha kutoa onyo, kusitisha ruzuku, na sasa hata kuzungumzia uwezekano wa kusimamisha usajili wa chama.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Wapinzani na wanaharakati wamekuwa wakikosoa sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2024, inayompa Msajili nguvu kubwa ya kuingilia mambo ya ndani ya vyama.
Tangu ukiwa katika hatua za mswaada, asasi za kiraia pia ziliikosoa sheria hiyo. Kundi lililojumlisha Twaweza, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Baraza la habari Tanzania (MCT), Centre for Strategic Litigation, Chama cha Waandishi wa Habari wa Maendeleo Zanzibar na Tanganyika Law Society lilisema sheria hiyo itakwenda kubadili majukumu ya msingi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
Madai yao yanajikita kusema Ofisi hiyo imetoka kuwa"msajili" mpaka kuwa "mdhibiti" na hapo ndipo mwanzo wa mahusian ya paka na panya yanapoanzia kati ya ofisi
📌 Kaynak
Bu özet BBC Swahili kaynağından otomatik derlenmiştir. Tamamı için orijinal habere gidin.
Orijinal haberi oku →