Kutafuna chakula vizuri kunaimarisha ubongo wako - Utafiti
Kutafuna zaidi kunaweza kutoa faida nyingi, kutoka kwa kuboresha usagaji chakula na kusababisha ulaji wa chini wa kalori, kupunguza mafadhaiko na wasiwasi, na kuboresha uwezo wa utambuzi kwa kuimarisha ustadi wa kumbukumbu na kuongeza muda wa umakini.
Horace Fletcher, aliyeishi mwishoni mwa karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20, alipewa jina la utani "Mtafunaji Mkuu" kwa sababu alitafuna shallot (aina ya kitunguu inayofanana na kitungu saumu) mara 722 kabla ya kuimeza.
Mtaalamu huyo wa lishe wa Marekani aliyejifundisha fani hiyo aliamini kwamba chakula kinapaswa kutafunwa hadi "kiwe laini kabisa" kiasi cha "kumezwa kwa urahisi."
Fletcher alikadiria kuwa kutafuna kabisa kungelisaidia kuokoa uchumi wa Marekani wa mwanzoni mwa karne ya 20 zaidi ya dola nusu milioni kwa siku (takriban dola milioni 19.5 za leo), kwa sababu mtu wa kawaida angetumia gramu 227 za chakula kwa siku.
Mafundisho ya Fletcher huenda yamepita kiasi, lakini "Kwa kiwango fulani alikuwa sahihi," anasema Mats Trulsson, profesa na daktari wa meno katika Taasisi ya Karolinska nchini Uswidi.
Kutafuna chakula vizuri kunaweza kuwa na manufaa kadha wa kadha, ikiwa ni pamoja na kuboresha usagaji chakula na kusababisha ulaji wa chini wa kalori, kupunguza mafadhaiko na wasiwasi, na kuboresha uwezo wa utambuzi kwa kuimarisha ustadi wa kumbukumbu na kuongeza muda wa umakini.
Kwa kuwa kuna uhusiano kati ya afya ya meno na ugonjwa wa Alzheimer na tatizo la ya kiakili, baadhi ya wataalam wanasema kuwa kuboresha afya ya meno ya wagonjwa kunaweza hata kusaidia kupunguza kasi ya kuzeeka kwa akili.
Adam van Casteren, mwanabiolojia katika Taasisi ya Max Planck ya Anthropolojia ya Mageuzi huko Leipzig, Ujerumani, anasema kwamba kama wanyama wengine, wanadamu " wamekuwa na meno kwa mamilioni ya miaka." lakini, walipata mabadiliko mengi katika nyakati za kabla ya historia.
Binadamu wa kale, walioishi takriban miaka milioni sita hadi saba iliyopita, walikuwa na meno sawa na ya nyani wa kisasa.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Van Casteren anasema, "yaliwasaidia sana kula ''matunda makubwa'' ambayo yalikuwa mengi katika maeneo ya misitu ambapo babu zetu wa kale waliishi."
Kulingana na Van Casteren, mvua ilipokuza misitu mingi, makazi wazi, na hata ikolojia kama savanna, binadamu wa kale walilazimika kula "vyakula vyenye changamoto zaid kutafuna" kama vile mbegu, njugu, na mizizi.
Kwa hiyo, ni meno yao yalibadilika na kuwa mapana, makubwa, ili kukidhi ongezeko la ukubwa wa meno hayo nakubwa na nyuso ili kushughulikia meno haya yote, pamoja na misuli kubwa inayohitajika kuziendesha.
Meno hayo yaliwawezesha kusaga,chakula kabla hakijamezwa ili kiwe rahisi kwa usagaji wa tumbo
Van Casteren anasisitiza kwamba ukuaji wa teknolojia, usindikaji wa chakula, na kilimo, pamoja na moto wa kupikia chakula, hitaji l
📌 Kaynak
Bu özet BBC Swahili kaynağından otomatik derlenmiştir. Tamamı için orijinal habere gidin.
Orijinal haberi oku →