Tunasitisha mashambulizi dhidi ya Israel, lakini tutaanza tena iwapo Israel itaishambulia Lebanon - Iran
Israel ilifanya mashambulizi ya anga dhidi ya Iran baada ya Tehran kuanza kurusha makombora kuelekea Israel siku ya Jumapili. Awali Donald Trump alizitaka nchi zote mbili "kusitisha mapigano".
Rais wa Iran amesema nchi hiyo "haijasitisha inachofanya wala kuondoka kwenye meza ya mazungumzo".
Masoud Pezeshkian anasema katika chapisho kwenye mtandao wa X kwamba kipaumbele cha nchi ni "usalama wa taifa na amani ya watu wetu", akiongeza kwamba "haitabadili msimamo kwa sababu ya tishio lolote".
Maoni hayo yamekuja baada ya kamanda mkuu wa kijeshi wa Iran Khatam al-Anbiya kutangaza kusitisha "shughuli zake za kijeshi", na kuongeza kwamba itajibu "vikali na kwa nguvu kubwa zaidi kuliko hapo awali" ikiwa mashambulizi yataendelea.
Wakati huo huo, Shirika la Viwanja vya Ndege na Urambazaji wa Anga ya Iran imesema katika taarifa kwamba safari zote za ndege nchini Iran zimefutwa hadi itakapotangazwa tena.
Msemaji wa Shirika la Usafiri wa Anga la Iran alitangaza jana usiku kwamba sehemu ya magharibi ya anga ya nchi hiyo imefungwa.
Iran ilikuwa imeanza kurejesha baadhi ya safari zake za ndege za abiria kuanzia mwishoni mwa mwezi Aprili, kufuatia makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Iran na Marekani tarehe 8 Aprili.
Nchi hiyo ilikuwa imefunga anga yake kwa kiasi kikubwa baada ya mashambulizi ya Marekani na Israel tarehe 28 Februari wakati vita vilianza.
Baadhi ya viwanja vya ndege vya Iran, ikiwemo Mehrabad ya Tehran, kushambuliwa wakati wa vita.
Tunasitisha mashambulizi dhidi ya Israel, lakini tutaanza tena iwapo Israel itaishambulia Lebanon - Iran
Israel imesema imefanya mashambulizi ya anga yaliyolenga maeneo ya magharibi na katikati ya Iran
📌 Kaynak
Bu özet BBC Swahili kaynağından otomatik derlenmiştir. Tamamı için orijinal habere gidin.
Orijinal haberi oku →